NENO LA FARAJA!
Neno la MUNGU linahuisha; maana ndani yake ipo faraja!
"Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu. Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo" (2Kor.3-5)!
Wapendwa, kwa mwanadamu anayeishi katika ulimwengu huu uliojaa dhiki, kitu pekee kitakachomwezesha kufurahia maisha ni Tumaini!. Je, TUMAINI latoka wapi?? Kwa nini baadhi yetu tunakosa hilo TUMAINI??
Ni katika kufarijia tunapeana TUMAINI, mojawapo ya zile fadhila kuu tatu za Kimungu (Imani, Matumaini na Mapendo).
Bwana wetu Yesu Kristo anasema "duniani mnayo dhiki, lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu" (Yon.16:33).
Ni kwa njia ya kufarijia tunajenga tumaini ambalo kwa hilo tunajipa moyo, na ni katika kujipa moyo tunaweza kupambana na dhiki za ulimwengu huu!
Ni kwa njia ya kufarijia tunajenga tumaini ambalo kwa hilo tunajipa moyo, na ni katika kujipa moyo tunaweza kupambana na dhiki za ulimwengu huu!
Ni wajibu wangu mimi kuwa sababu ya faraja kwako; ni wajibu wako wewe kuwa sababu ya faraja kwangu.
Faraja kuu inatoka kwa MUNGU; lakini sisi ni sura na mfano wa MUNGU. Hatuwezi kumwona MUNGU kwa sura na mfano mwingine isipokuwa kupitia binadamu aliyemuumba ambaye ni mimi na wewe!
Anza sasa kuwa faraja kwa wengine ili uwe wakili mzuri wa MUNGU mfariji! Umeshafarijiwa na MUNGU kupitia wengi, nawe wafariji wengi zaidi!
"NI HERI KUFARIJI KULIKO KUFARIJIWA"!
By
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni