Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Francisco
Montecillo Padilla, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Kuwait na mjumbe wa
kitume kwenye Kisiwa cha Kiarabu. Itakumbukwa kwamba, kabla ya uteuzi huu,
Askofu mkuu Francisco Padilla alikuwa ni Balozi wa Vatican
nchini Tanzania!
Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla alizaliwa kunako tarehe
17 Septemba 1953 Jijini Cebu, Ufilippini. Baada ya masomo na majiundo yake ya
kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 21 Oktoba 1976. Tarehe
1 Aprili 2006 akateuliwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Papia New
Guinea na Visiwa vya Solomon. Tarehe 23 Mei 2006 akawekwa wakfu kuwa Askofu
mkuu. Tarehe 10 Novemba 2011 akateuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI
kuwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania!
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
Related Posts
- MAPADRI HESHIMUNI SADAKA ZA WAAMINI12 Jan 2018Maoni
PAROKO wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeli jimboni Morogoro Padri Vivian Menezes, amewaasa mapadri nchini kushika njia ya utakatifu na kutham...Read more »
- WAZAZI WAWE MAKINI NA VIPINDI VYA LUNINGA KWA WATOTO12 Jan 2018Maoni
Na Angela Kibwana, Morogoro ASKOFU wa Jimbo Katoliki Morogoro Mhashamu Telesphor Mkude amewaonya baadhi ya wazazi wenye tabia ya kuwaacha watoto ...Read more »
- Maaskofu watoa ujumbe wa Kwaresima 20111 Feb 2018Maoni
MAASKOFU 35 wanaounda Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wametoa ujumbe wa Kwaresima kwa 2018, huku wakiwataka waamini wakatoliki wote kuuitik...Read more »
- 20 Nov 2017Maoni
Tabia ya Baba Mtakatifu katika mawasiliano daima ni nyepesi, mtazamo na ishara zake ndiyo mtindo wake. Ni maneno ya Monsinyo Dario Vigano’ Mwenyek...Read more »
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni