0


Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa hii majira ya adhuhuri,   alipokea Tuzo ya Kimataifa ya Charlemagne kutoka kwa ujumbe wa Bunge la Ulaya wakiwa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Baraza la Ulaya Donald pembe, Martin Schultz na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker.Tuzo hiyo imetolewa kwa Papa kama kutambua juhudi zake katika kutetea Umoja na haki barani Ulaya. 
Katika hotuba yake, Papa Francis amesisitiza iwapo Ulaya inapenda kuendeleza heshima na mustakabali wa amani, kwa siku za baadaye katika jamii ya Ulaya , inawezekana tu kuwa hivyo, kwa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu,  wenye kuwajumuisha wote.
Na kwamba, kwa ajili ya kuleta moyo mpya kwa ulaya inayoonekana kuchoka, ingawa  bado ina nguvu nyingi na uwezekano, Kanisa linaweza na lazima lifanye sehemu yake. Papa Francisko ametaja moja ya utume wake  Kanisa ni kutangaza Injili , ambayo leo hii kuliko hata ilivyokuwa siku za nyuma,ni kuhimiza maisha ya kutoka na kwenda  kufunga majeraha ya binadamu aliyejeruhiwa, kwa nguvu nyepesi ya kusadiki  uwepo wa Yesu, na huruma yake kwamba huleta faraja kwa mioyo iliyopondeka. 
Baba Mtakatifu Francisko majira ya saa sita mchana, alipokea kundi la uwakilishi toka Bunge la Ulaya, waliofika Vatican kwa lengo la kumkabidhii tuzo ya mwaka huu ya Bunge la Ulaya ambayo hutolewa kwa mtu aliyeonyesha juhudi zaidi katika kutetea haki na umoja barani Ulaya. Kwa mwaka huu, Tume inayohusika na kuchagua mshindi wa Tuzo , ilimchagua Papa Franciko, kuwa ndiye ameng’ara zaidi katika kutetea haki na umoja wa Ulaya. , 
Hotuba ya Papa , iliendelea kuhimiza Umoja wa Ulaya uendelee kuwa fikra za ubunifu katika  uwezo wa kuanza upya katika kufanya mabadiliko chanya katika nafsi ya watu wa Ulaya. Na aliitazama historia ya Ulaya ambayo inaonyesha kwamba, karne iliyopita, Ulaya aliweza kuthibitisha kwamba daima inawezeakana kuwa na mwanzo mpya katika kujenga ubinadamu wenye kuzingatia mazuri, baada ya miaka ya migogoro ya kutisha, iliyofikia katika upeo wa vita ya kutisha, lakini kwa  neema ya Mungu, waliweza kuanza tena upya  kabisa katika historia ya binadamu. Na kwamba vifusi na  majivu ya magofu hakuweza kuzima moto wa matumaini ya  wakereketwa  waanzilishi wa  jitihada za  kuanzisha tena na umoja na mshikamano wa watu wa Ulaya. . Wao waliweza kuweka misingi ya ngome ya amani, katika kujenga umoja wa  mataifa, umoja si kwa manufaa yao binafsi  lakini kwa dhamira ya manufaa ya wote. Ulaya, iliyokuwa imegawanyika kwa  muda mrefu , hatimaye  ikafuta hali hiyo na kuanza kujenga nyumba yake mpya  katika umoja. .
Hotuba ya Papa ilieleza na kutoa mifano mingi ya  kihistoria kama ilivyonukuliwa na waandishi na wadhamini wa kidini  mbalimbali hatimae akasema kumbukumbu hizi na ziwawezeshe kwa wakati huu , kuleta msukumo mpya  katika kukabiliana kwa ujasiri  na mfumo wa uharibifu  ulioenea katika  siku hizi  zetu wenyewe. Ni lazima kuwa na hatua za kujituma na kutoa changamoto katika kuleta upya na kuimarisha zaidi na zaidi Umoja wa  Ulaya.  Papa ameonyesha tumaini lake kubwa kwamba, Ulaya  ina uwezo wa kufungua utu mpya unaotokana na  uwezo wa Ulaya katika mambo matatu: uwezo wa kuunganisha, uwezo katika mazungumzo na uwezo wa kuzalisha.  Na kwamba  anayo matumaini yote kwamba,  Ulaya itaweza kudumisha na kulinda haki za kila mtu, bila kusahau majukumu yake katika  kusaidia wahitaji zaidi. 

Chapisha Maoni

 
Top