Mapokeo
Matakatifu,Ndoa ya Bikira Maria haiwezi kutoshelezwa na maelezo kutoka kwenye
Biblia.Inabidi kuwauliza wale walioishi naye ili tuweze kupata habari za maisha
yake.Hapa ndipo umuhimu wa mapokeo Matakatifu unapoonekana.Kuhusu umuhimu wa
Mapokeo Matakatifu(SomaYeremia6:16,Kumbukumbu la
Torati32:1-12,Yohane20:30,Yohane21:25,Luka1:1-3 na 2Wathesalonike3:6-7).Ndugu
zangu tusiyadharau Mapokeo Matakatifu ndio yaliyozaa Biblia.Kwa hiyo huwezi
kuyahukumu Mapokeo Matakatifu kwa kutumia Biblia.Na Mapokeo Matakatifu ya
Kanisa Katoliki yanaonesha Bikira Maria hakupata watoto wengine zaidi ya Yesu.
3.Matumizi
ya jina Maria,Kuna wakina Maria chungu nzima kwenye Biblia.Kuna Maria wa
Bethania(Yohane11:1-3),Maria mama yake Yohane,Huyu ndiye mama aliyempokea mtume
Petro alipotoka gerezani(Matendo ya Mitume12:12),Maria
Magdalena(Matayo28:1-8),Maria wa Roma(Warumi16:6),Maria mama yake Yakobo
mdogo,Yose na Salome(Marko15:40),Maria Mama yake Yesu(Yohane19:25-27,Matendo ya
Mitume1:14).Kwa hiyo ndugu zangu inabidi kujua yupi ni Maria mama yake Yesu
ukilinganisha na wakina Maria wengine.Jina Maria limetafsiriwa kwa maana nyingi
lakini maana inayokubalika na wengi ni "Kipenzi cha Mungu".Jina
"Maria asili yake ni lugha ya "Kilatini",Miriam
kwa"Kiebrania" na Mariam kwa "Kiaramayo".Majina haya yote
yana maana sawa
Ndugu
zangu aya za Biblia zinazoibua swali hilo
ni(Matayo1:25,Marko6:1-6,Matayo12:46-50,na Luka8:19-21).Hizi aya ukizisoma zinataja
kaka na dada za Yesu.Waweza kujiuliza hao kaka na dada za Yesu wanaotajwa
kwenye aya hizo hapo juu ni kaka na dada zake wa damu?Ndugu yangu uliyeuliza
hili swali,Ndoa ya Bikira Maria ilikuwa ya ajabu mno.Tunasema ilikuwa ya ajabu
sababu alipata mimba pasipo tendo la ndoa.Maria akamwambia Malaika
"Litakuwaje neno hili maana mimi sijui mume?Luka1:34).Bikira Maria alipata
mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.Kwa kuonesha Bikira Maria alipata mimba kwa
uwezo wa Roho Mtakatifu soma Injili ya Luka1:35).Kanisa Katoliki linafundisha
Bikira Maria hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu kwa kutumia hoja
zifuatazo;1-Mila na desturi za Kiyahudi,Kwa Wayahudi suala la kuitana kaka na
dada lilikuwa jambo la kawaida kama kwenye mila na tamaduni zetu za
kiafrika.Mtu kumwita dada haina maana kwamba mlizaliwa tumbo moja.Au kumwita
mtu fulani mama,baba au ndugu si lazima awe ndugu wa damu.Neno la
Kigiriki"Adelphoi"kwa mwanaume na "Adelphai" kwa
mwanamke.Maneno hayo yanaweza kutafsiriwa kama ndugu wa damu mfano
kaka,dada,ndugu wa kambo mfano kaka au dada.Neno hilo laweza kutafsiriwa pia
kama jamaa,jirani au rafiki.Kwa hiyo Biblia inapotaja ndugu au kaka na dada
zake Yesu Kristo haina maana ya ndugu wa damu bali yaweza kuwa jirani,jamaa au
rafiki.Waweza kurejea undugu wa Abrahamu na Lutu haukuwa undugu wa damu lakini
wao wanaitana ndugu (soma Mwanzo13:8,Walawi10:4-5).
4-Wajibu
wa watoto wa Kiisraeli,watoto wa Kiisraeli waliwajibika kuwatunza wazazi wao
wanapozeeka au mmojawapo anapofariki.Kitendo cha Yesu kumkabidhi mama yake kwa
mwanafunzi aliyempenda(Mtume Yohane) kinaonesha wazi kabisa Bikira Maria hakuwa
na mtoto mwingine zaidi ya Yesu.Kama Bikira Maria angekuwa na watoto wengine
zaidi ya Yesu,Yesu mwenyewe asingethubutu kumkabidhi mama yake kwa mwanafunzi
aliyempenda sababu ingetafsiriwa kama dharau kwa wadogo zake na kuwakosesha
heshima katika jamii ya Kiisraeli sababu wao ndio walikuwa na wajibu wa
kuwatunza wazazi wao.Hata katika tamaduni zetu za kiafrika,Baba akifariki
watoto wanakuwa na wajibu wa kumtunza mama.Inasikitisha sana baba yako
anafariki halafu mama yako unamkabidhi rafiki yako amtunze wakati wewe na
wadogo zako mpo.Hii inaingia akilini kweli?wewe mwenyewe unayo majibu.Pia kama
Bikira Maria angekuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu,Mbona msalabani
hawakuonekana?Kitendo cha Yesu kumkabidhi mama yake kwa mwanafunzi aliyempenda
ilionesha wazi kabisa hata mume wake Mtakatifu Yosefu alikuwa ameshafariki.Kama
Yosefu ambaye ni baba mlishi wa Yesu angekuwa hai,Yesu asingethubutu kumdharirisha
baba yake kwa kitendo cha kumkabidhi mama yake kwa mwanafunzi
aliyempenda.Waweza kujiuliza kama Yosefu alikuwa ameshafiriki,Bikira Maria
alizaa na nani?Na Yosefu angekuwa hai kipindi hicho tungemwona msalabani.Kwa
hiyo ni hakika alikuwa ameshakufa (Yohane19:25-27).Kwa hoja hizo mnamo mwaka
553 huko Konstantinopoli,Mama Kanisa Mtakatifu sana alitangaza fundisho la
kiimani(Dogma) kwamba,Bikira Maria mama wa Mungu(Theotokos) alikuwa Bikira
kabla ya kumzaa Yesu(Ante partum-Kilatini),Alikuwa Bikira wakati wa kumzaa
Yesu(In partum kwa Kilatini),na Alikuwa Bikira baada ya kumzaa Yesu (Post
partum kwa kilatini).Kitendo cha Bikira Maria kumzaa Yesu hakikupunguza wala
kuharibu ubikira wake bali kiliutakatifuza ubikira wake.(Rejea hati ya Mtaguso
wa ll Vatican,Constitutio ya kidogma juu ya fumbo la Kanisa"Lumen Gentium
No.53.Pia Jalimu la Maandiko Matakatifu(The Father of Biblical Science)
Mtakatifu Jerome(437-420) alitafsiri Isaya7:14 kwa kutumia neno la
Kiebrania"Alma" kuonesha kwamba Bikira Maria ni msichana ambaye ubikira
wake umefichwa au wa siri.Ndio maana hata Kanisa Katoliki humwita Bikira
Maria"Alma Mater" yaani Bikira aliye wa siri au aliyefichwa.Kwa hiyo
Bikira Maria hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu.Kaka na dada wanaotajwa
kwenye Biblia inawezekana kabisa walikuwa watoto wa akina Maria wengine lakini
si Maria mama yake Yesu.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni