Kwa furaha kubwa ninawakaribisheni muda huu mkiwa ukingoni mwa hija yenu katika maeneo ya Roma, iliyo andaliwa na Baraza la Kikapapa kwa ajili ya Maaskofu na Makanisa ya Mashariki. Shukrani pia zimwendee Kardinali Marc Quellet na Kardinali Leonardo Sandri ambao ni Wenyeviti wa mabaraza hayo ya kipapa kwa jitihada zao za kuwezesha tukio hili ambalo ninalitambua binafsi, kutokana na hawa wachungaji wapya wa Kanisa kuweza kujikita kwa undani na kutafakari neema na wajibu wa kitume tulio upokea.
Ni utangulizi wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 14 Septemba 2017 alipokutana na Maaskofu waliowekwa wakfu kwa siku za hivi karibuni wakiwa katika hija ya pamoja mjini Vatican. Kwa hakika anasema, siyo katika mashaili yao bali ni kwa neema ya Mungu ambaye amewakabidhi ushuhuda wa Injili ya neema ya Mungu na utume wa Roho yake. Mpango wa hija yenu mwaka huu Roma Baba Mtakatifu anasema, umejikita katika kutafuta na kuingia kwa undani zaidi wa fumbo ambayo ni mojawapo ya wajibu msingi ule wa kujitoa kabisa katika zizi kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye aliwaweka kama walinzi (At 20,28), katika mang’amuzi ya kiroho na ulazima wa uchungaji ili kuwa na utambuzi na kutimiza kwa njia ya mapenzi ya Mungu ambaye ni kisima cha neema.
Baba Mtakatifu Francisko anaomba kushirikisha zaidi juu ya mambo kadhaa ya tafakari kuhusu mada hiyo ambayo ni muhimu sanakwa nyakati hizi. Anasema, nyakati hizi ni zile zinazoenekana alama ya binadamu kupenda kujitegemea na kujitosheleza na kutangaza mwisho wa kipindi cha ualimu katika upweke wake. Lakini hiyo inaonekana wazi kuwa, binadamu kamili bado anaendelea kupiga kelele ili aweze kusaidiwa kukabiliana na matazizo yanayo msonga, na ili aweze kuongozwa katika njia ambayo kwa dhati ni changamoto kwake na hatimaye aweze kuandaa utume wake katika kutafuta maisha yake ya furaha. Hiyo ni dhahiri ya mang’amuzi ambayo Mtakatifu Paulo anawasilisha kama mojawapo ya zawadi za Roho Mtakatifu, na Mtakatifu Tomas wa Aquinas anaita uadilifu mkuu ambao unahukumu kwa mujibu wa misingi mikuu na ambayo tunaweza kujibu mahitaji ya binadamu wa leo.
Roho Mtakatifu ni kiongozi wa kila aina ya mang’amuzi ya dhati, kwasababu siyo siku nyingi zilizopita , Kanisa limesali kwa ajili yenu kwake Roho wa Bwana ambaye ni msingi na nguvu ambayo Baba alimpatia mwanae na yeye mwenyewe akawapatia mitume wake, maana yake ni Roho ambaye anasisimamia na kuongoza.
Kwa njia hiyo ni lazima kutambua zawadi hiyo ambayo daima wote ni wahudumuwake na daima tumepokea juu ya mabega yetu dhaifu. Baba Mtakatifu anaongeza kusema, labda ndiyo maana Kanisa wakati wa sala ya kumweka wakfu Askofu, waliweza kuchukua Zaburi ya huruma ambayo mzaburu anaelezea historia yake mara baada ya kushindwa kabisa kutokana na dhambi zake, anasali kwake Roho Mtakatifu amjalie wema katika utii na Mungu. Lakini huo ndiyo msingi kwa yule anayeongoza jumuiya yoyote anasisitiza Baba Mtakatifu
Anayeweza kufundisha na kukua katika ufahamu ni yule tu anayejifunza kutoka kwa mwalimu, ni mwalimu wa ndani kama dira. Ni yule anatoa vigezo vya kutofautisha kwa ajili yake na wengine nyakati za Mungu na za neema yake. Anauweza kuwa kuonesha nyenzo halisi za kumpendeza Mungu ili kukamilisha mema ambayo Yeye hutangulia katika mpango wake wa ajabu wa upendo kwa kila mmoja na kwa wote. Ni wale ambao wanaongozwa na Mungu wana cheo na mamlaka ya kupendekezwa kama viongozi wa wengine. Hekima hii ni hekima ya msalaba pamoja na kujumuisha sababu na busara, inapita zaidi kwasababu inaongoza kwenda katika kisima cha maisha yenyewe ambayo hayafi tena na kumjua Baba Mungu pekee wa kweli na yule aliyetumwa Yesu Kristo.
Askofu hawezi kujishughulisha kutoa hivi hivi zawadi kubwa kutoka juu kama kwamba alikuwa na haki ya kuipata, bila kuangukia katika huduma isiyo zaa matunda. Ni muhimu kuendelea kuomba kwa jambo msingi katika kuangaza kila mtu hekima. Hekima ya kijamii , hekima ya maadili, hekima ya kisaikolojia ambayo inaweza kutumika katika kazi ya utambuzi wa njia za Mungu kwa ajili ya wokovu wa wale ambao tumepewa.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anasema, ni lazima kurudia kuomba tukikumbuka Bwana anavyosema, ni kama watoto ambao hawajuhi kujipima, kuomba siyo siku chache za kuishi, siyo utajiri na wala maisha ya maadui wetu , bali ni lazima kuomba hekima ya maang’amuzi ya kuhukumu kati ya watu wake. Bila neema hii, hatuwezi kuwa wataalamu wa vipima joto ambao wanaweza kuona kile kitakachoonekana katika hanga, lakini hawna uwezo kutathmini wakati wa Mungu.
Mang’mauzi kwa njia hiyo yanatoka katika moyo na akili ya Askofu kwa njia ya sala na kujikita kwa kina, aidha kuwasiliana hata ma watu ambao tumepewa kuwaongoza na kwa njia ya Neno la Mungulitokanalo na Roho. Ni katika urafiki huo kwamba Mchungaji anakomaa kwa uhuru wa ndani na kumfanya awe imara katika uchaguzi na tabia na mwendendo wake binafsi kama ule pia wa Kanisa .
Katika utulivu wa maombi unaweza kujifunza sauti ya Mungu, kutambua matukio ya lugha yake, upatikanaji wa ukweli wake, ambao ni mwanga tofauti sana. Baba mtakatifu anatoa mfano kuwa haupo juu ya akili kama mafuta yanayoelea juu ya maji na wala zaidi lakini ni yule anaye jua ukweli wa Mwangu huu. Ni katika utulivu wa sala unaweza kujifunza sauti ya Mungu na kutamba neema ya Roho Mtakatifu katika Kanisa ambaye anasikiliza.
Baba Mtakatifu francisko amemaliza hotuba yake akiwaomba wawe karibu sana na Yesu na kuwatunza kondoo wao waliopewa. Wawe na nafasi ya kukutana na Mungu na kuchagua njia zake wakiendelea mbele na upendo wake. Aidha akikumbuka sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba, anasema wadumu na kuwa na ufahamu wa Mungu kwa kutafakari kwa kina juu ya mwili wa mwanae Yesu Kristo, zaidi katika kigezo cha kutokumsadiki kila mtu asemaye kwamba ana roho wa Mungu, bali wachunguze kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni. (1 Yohana 4: 1) . Amemaliza hotuba yake akiwabariki na kubariki Makanisa yao wanakotokea.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni