0
Kuna Wakristo wa Agano jipya kama mimi, wanamwamini Mungu na Neno lake, lakini wamekuwa wakipata wakati mgumu kuhusu swala la FUNGU LA KUMI kama ni sahihi kwa WATU WA AGANO JIPYA KUTOA AINA HII YA SADAKA, AU KAMA ILIKUWA IKIWAHUSU WAISRAELI PEKE YAO KAMA SEHEMU YA SHERIA ALIZOPEWA MUSA NA MUNGU… Hapa ni muhimu tupitie BIBLIA na kujua kweli kadhaa zitakazokusaidia kuwa MTOAJI WA FUNGU LA KUMI[ ZAKA] mwenye kuona MATOKEO NA NGUVU ZAKE KWENYE UCHUMI WAKO NA MAISHA YAKO KWA UJUMLA!


1.FUNGU LA KUMI NI NINI
Ni sehemu ya kumi [10%] ya mapato yako. Wengi wanadhani wanapaswa kutoa 10% ya mishahara yao au pesa ya faida ya biashara zao tu… Hii si kweli, KILA PESA INAYOPITIA MKONONI KWAKO; Hata kama ni pocket money umepewa na mzazi, au ndugu au rafiki amekupatia, SI MSHAHARA TU…NARUDIA KUSEMA SI MSHAHARA TU… MIMI NILIANZA KUTOA FUNGU LA KUMI TOKA KWENYE POCKET MONEY, NA PESA NILIZOKUWA NIKIPEWA NA NDUGU AU MARAFIKI NIKIWA KIDATO CHA PILI KULE SEKONDARI YA WAVULANA TABORA, BAADA YA MUNGU KUYAFUNGUA MACHO YANGU YA ROHO KUHUSU KANUNI HII YA MUHIMU KWA RAIA YEYOTE WA MBINGUNI.
FUNGU LA KUMI AU ZAKA KWA MKRISTO AU RAIA WA UFALME WA MUNGU SI SWALA LA HIARI, NI SHERIA NA LAZIMA, FUNGU LA KUMI NI KODI YA MUNGU…Anachukua 10% ya kila anachokupatia…wewe unabaki na 90% lakini bado Wakristo wengi wamekuwa WAKIMUIBIA MUNGU KODI YAKE…Kwenye kitabu cha MALAKI 3:8-11 Mungu anawaita wote wasiotoa FUNGU LA KUMI NA DHABIHU KUWA NI WEZI…Soma na ujionee!

2.FAIDA ZA KUTOA FUNGU LA KUMI
MALAKI 3:8-11 Mungu anaeleza wazi FAIDA NA UMUHIMU WA KUTOA FUNGU LA KUMI/ ZAKA, NAZO NI;
a)UNAMUWEKA MUNGU KAZINI KULINDA UCHUMI WAKO NA MFUMO WAKO WA KIFEDHA
b)KUPITIA FUNGU LA KUMI UNAFANYA AGANO NA MUNGU, NA UNAJENGA USHIRIKA NA KULIWEKA KUMBUKUMBU LAKO MBELE ZA BWANA
c)UNAMFUNGULIA MUNGU MLANGO NA NJIA YA KUPITISHIA BARAKA ZAKE ZA MJINI NA MASHAMBANI ILI AZIJAZE HAZINA ZAKO HATA ISIWEPO NAFASI YA KUTUNZA BARAKA HIZO
d)UNAMWEKA MUNGU KAZINI KUSHUGHULIKA NA MAISHA YAKO NA YA WATU WAKO

3.UMUHIMU WA FUNGU LA KUMI
a)FUNGU LA KUMI NI NJIA YA KIBIBLIA NA KANUNI YA UFALME WA MUNGU INAYOTUMIWA NA MUNGU KUIENDELEZA [ KUI-SUPPORT] KAZI YAKE NA SHUGHULI ZA UFALME WAKE
b)NI NJIA YA MUNGU KUWATUNZA WATUMISHI WAKE/ MAKUHANI NA WALAWI (WATUMISHI KWA UJUMLA)…Hebu fikiria mtumishi wa Mungu anayekulisha wewe vya rohoni, ambaye anakaa miguuni kwa BWANA kutafuta majibu ya maisha yako, ambaye ni FULL TIME MINISTER, Unataka ale wapi? Mungu ameweka FUNGU LA KUMI kama sehemu yao ya kuendeshea maisha yao…Je ingekuwaje Mchungaji wako aache kuomba na kusimamia kazi ya Mungu naye atafute pesa na maisha kama wewe, hasara ngapi utapata na kwa kiasi gani Mungu na Ufalme wake utapata shida? Ndio maana kati ya vitu ambavyo SHETANI ANAPIGIA KELELE SANA KUPITIA VINYWA VYA WATU NI FUNGU LA KUMI…Utasikia, oooh Mtumishi fulani anajilimbikizia mali, anaweka wapi hilo fungu la kumi nk…lakini hapa kuna angalizo, kwa makanisa na huduma kubwa; NI VEMA WATUMISHI WAKAOMBA HEKIMA YA NAMNA YA KUGAWA HELA YA FUNGU LA KUMI KWA AJILI YAO NA PIA KU-SUPPORT HUDUMA.

4.JE FUNGU LA KUMI [ZAKA] IMEANZA WAKATI WA MUSA KAMA SHERIA?
Wakristo wengi wa AGANO JIPYA wanadhani hii ilikuwa sheria ya AGANO LA KALE iliyowahusu Waisraeli. Lakini Ukweli ni kwamba FUNGU LA KUMI AU ZAKA HAIJAANZA KWENYE ZILE AMRI ALIZOPEWA MUSA…Mtu wa kwanza aliyerekodiwa kwenye BIBLIA KUTOA FUNGU LA KUMI ni IBRAHIMU (MWANZO 14:18-19)… Hii ilikuwa ZAIDI YA MIAKA 430 kabla ya TORATI NA SHERIA… UKISOMA BIBLIA YAKO UTAONA UKWELI HUU

5.JE FUNGU LA KUMI NI FUNDISHO LINALOTUHUSU WATU WA AGANO JIPYA? AU ILIKUWA KWA WATU WA AGANO LA KALE TU?
Jibu la swali hili ni kuwa FUNGU LA KUMI SI SHERIA YA TORATI, NI MFUMO WA UFALME WA MBINGUNI, AMBAO MUNGU ANAUTUMIA KUYAFANIKISHA MAISHA YA WOTE WALIO NA AGANO NAYE…Sisi pia tuna AGANO NA MUNGU, AGANO LILILO BORA, AGANO JIPYA, TULILOLIPATA PALE MSALABANI KWA DAMU YA YESU… YESU KRISTO NDIYE ALIYE KUHANI MKUU KWA MFANO WA MELKIZEDEKI, NI KUHANI WA MILELE AMBAYE ANAPOKEA MAFUNGU YA KUMI YA WAKRISTO, WATU WALIO NA AGANO NAYE KWA DAMU YAKE YA THAMANI…Hivyo basi unapotoa FUNGU LA KUMI usije ukafikiri ya kuwa UNAMSAIDIA MUNGU NA UFALME WAKE…HAPANA, MUNGU ANAWEZA KUGHARAMIKIA KAZI YAKE, ILA AMEWEKA NJIA HII KWA AJILI YA USTAWI WAKO NA ILI APATE MAHALI AU NJIA YA KUKUFANIKISHA…UNAPOTOA FUNGU LA KUMI UNATENGENEZA UHALALI WA KIAGANO NA MUNGU WA KUPOKEA FAIDA NA BARAKA ZINAZOAMBATANA NA SADAKA HII… Unapotoa FUNGU LA KUMI usije ukadhani unamsaidia Mtumishi wa Mungu asife na njaa…Hapana, MUNGU ALIYEMLISHA ELIYA KWA KUTUMIA KUNGURU HAJABADILIKA, ANAWEZA KUFANYA HIVYO…MUNGU ALIYEWAPA ISRAELI KWARE NA MANA ANAWEZA KUWATUNZA WATUMISHI WAKE BILA FUNGU LAKO LA KUMI…AMEKUPA NAFASI YA UPENDELEO KUSHIRIKI BARAKA ZA KUUJENGA UFALME WAKE, MAANA WEWE NI MTENDA KAZI PAMOJA NAYE… Unapotoa FUNGU LA KUMI haupandi MBEGU, bali unampa MUNGU NAFASI YA KUKUPATIA MKATE NA DIVAI, kama alivyofanya kwa Ibrahimu toka mikononi mwa Melkizedeki (Mwanzo 14:18-19)….UNAKUWA UMELIPA KODI, UNAKUWA UMEMRUDISHIA MUNGU MALI YAKE… Kwa upande wangu, kwa neema ya Mungu, kwa sasa natoa 20% ya kila pesa inayopita mkononi kwangu, sijidhanii kwamba nimefika, naendelea kumsihi Mungu baada ya miaka michache ijayo niwe namrudishia Mungu 90% ya mapato yangu yote, na mimi nitumie 10% maana Yeye ni mwenye YOTE NIYAPATAYO, YEYE NDIYE ANAYEMILIKI VYOTE, MIMI NI MRITHI TU PAMOJA NA KRISTO YESU!

6.JE KUNA ANDIKO LA AGANO JIPYA LINALOZUNGUMZA KUHUSU FUNGU LA KUMI/ SEHEMU YA KUMI?
Ndiyo, Ukisoma kitabu cha Waebrania 7, Maneno; SEHEMU YA KUMI, FUNGU LA KUMI, ZAKA YAMETUMIKA ZAIDI YA MARA 4… Huu ni ushahidi tosha kuwa Fungu la kumi si sheria ya torati bali ni KANUNI YA MUNGU NA WALE ALIONAO KATIKA AGANO ILI KUWASAIDIA NA KUWASTAWISHA!

7.NAMNA SAHIHI YA KUTOA FUNGU LA KUMI/ ZAKA
Pale unapopata pesa mkononi mwako, iwe mshahara, au faida ya biashara au mifugo uliyouza… swala si kutoa kiasi cha 10% bali kinachougusa MOYO WA MUNGU ni KUTENGA FUNGU LA KUMI KWANZA KABLA YA KUITUMIA kufanya kingine chochote… Hata kama una madeni, au unatakiwa kulipa kodi, hakikisha kuwa unatoa kwanza FUNGU LA KUMI kabla ya kulipa hizo kodi na mahitaji!
UNAPOTOA FUNGU LA KUMI kwanza, unamaanisha ya kuwa Mungu ni wa kwanza kwako…Unapotumia kwanza na kuleta FUNGU LA KUMI mwishoni, unamaanisha MUNGU NI WA MWISHO KWENYE VIPAUMBELE VYAKO…Kinyume na MATHAYO 6:33

(Share kwa wingi uwezavyo ili kuwasaidia Wakristo wengine, na pamoja tutakuwa tumemtumikia Mungu )!


Chapisha Maoni

 
Top