SOMO 1
Nya. 24:17 – 25
Nya. 24:17 – 25
Baada ya kufa kwake Yehoyada, wakuu wa Yuda wakamwendea mfalme, wakamsujudia. Naye mfalme akawasikiliza maneno yao. Wakaiacha nyumba ya Bwana, mungu wa baba zao; wakatumikia maashera na sanamu; ghadhabu ikawajia Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hiyo hatia yao. Hata hivyo akawapelekea manabii, ili kuwarudisha kwa Bwana; nao wakawashuhudia; lakini hawakukubali kuwasikiliza.
Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za Bwana, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi. Basi, wakafanya shauri juu yake, wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme, katika ua wa nyumba ya Bwana. Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, Bwana na ayaangalie haya, akayatakie kisasi.
Ikawa mwisho wa mwaka, wakakwea juu yake jeshi la Washami; wakafika Yuda na Yerusalemu, wakawaangamiza wakuu wa watu wote miongoni mwa watu, wakamletea mfalme wa Dameski nyara zao zote. Maana wakaja jeshi la Washami watu haba; Bwana akatia mikononi mwao jeshi kubwa mno, kwa sababu wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao.
Hivyo wakamfanyia Yoashi hukumu. Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 89: 3- 4, 28 – 33 (K) 28
Zab. 89: 3- 4, 28 – 33 (K) 28
(K) Nitamwekea fadhili zangu milele.
Nimefanya agano na mteule wangu,
Nimemwapa Daudi, mtumishi wangu.
Wazao wako nitawafanya imara milele,
Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele. (K)
Nimemwapa Daudi, mtumishi wangu.
Wazao wako nitawafanya imara milele,
Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele. (K)
Hata milele nitamwekea fadhili zangu,
Na agano langu litafanyika amini kwake.
Wazao wake nao nitawadumisha milele,
Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. (K)
Na agano langu litafanyika amini kwake.
Wazao wake nao nitawadumisha milele,
Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. (K)
Wanawe wakiiacha sheria yangu,
Wasiende katika hukumu zangu,
Wakizihalifu amri zangu,
Wasiyashike maagizo yangu. (K)
Wasiende katika hukumu zangu,
Wakizihalifu amri zangu,
Wasiyashike maagizo yangu. (K)
Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo,
Na uovu wao kwa mapigo.
Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye,
Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo. (K)
Na uovu wao kwa mapigo.
Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye,
Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo. (K)
SHANGILIO
Zab. 119: 135
Zab. 119: 135
Aleluya, aleluya,
Umwangazie mtumishi wako uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
Umwangazie mtumishi wako uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
INJILI
Mt. 6: 24 – 34
Mt. 6: 24 – 34
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Hkuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongoeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasonkoti; nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
[6/17, 22:17] Nyambane Maurice: “ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Juni, 18, 2016,
Juma la 11 la Mwaka wa Kanisa
[6/17, 22:17] Nyambane Maurice: “ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Juni, 18, 2016,
Juma la 11 la Mwaka wa Kanisa
2 Nya 24: 17-25;
Zab 88: 4-5, 29-34;
Mt 6: 24-34
Zab 88: 4-5, 29-34;
Mt 6: 24-34
BWANA WANGU NINANI- MUNGU AU PESA?
“Moyo uliogawanyika ni moyo wa huzuni.” Wote tunajua hili kwasababu ni moyo ulio na wasi wasi na usiojiweza. Leo tunasikia Yesu akituambia hatuwezi kutumikia mabwana wawili. Hatuwezi kujitoa kwa Mungu moja kwa moja kama tumetekwa na pesa. Kwanini? Kwasababu vyote vinahitaji kujikita na kujitoa. Mungu anahitaji majitoleo ya kweli si kwaajili yake bali kwaajili yetu wenyewe. Hatuwezi kuwa na furaha kabisa au furaha ya kweli bila Mungu. Na ni Mungu mwenyewe anaweza kurudhisha tamaa ya moyo wa Mwanadamu.
Hakuna mtu anaeweza kuwatumikia mabwana wawili kwa muda mrefu. Kwasababu wakati Mabwana wote wawili wakiwa wanatembea pamoja, anaweza kuwafuata nyuma yao lakini watakapo amua mmoja kwenda uelekeo wake na huyu wake, lazima achague ni yupi wakumfuata. Haijalishi ni mara ngapi watu wamemuasi Mungu na kufuata au kuabudu mali na pesa, Mungu haachi kamwe kuwapigania warudi kwake. Tujikumbushe maneno haya ya Mungu “Sitawaacha kamwe wala kuwakataa ninyi” (Kumb 31: 6). Somo la kweli katika historia ya Mwanadamu ni kwamba-Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili katika hali ya kweli. Mkristo kwa kweli hawezi kutenda haki ya Mungu kwakujiingiza kabisa katika mali na anasa za ulimwengu huu.
Uovu wa kujaribu kugawanya uaminifu wetu unajikita katika kushindwa kwetu kutumainia Upendo wa Mungu Baba yetu. Tunajaribu kutafuta ulinzi wa maisha yetu katika mali na utajiri wetu. Tunafanya kila liwezekanalo kulinda heshima yetu katika mali, tunadhani tukipungukiwa tutadharauliwa na watu, kwahiyo siku zote tunajaribu kujilinda kuweka mambo yetu vizuri bila kujali kama na muumiza mwanadamu mwenzangu. Tunawatumikisha wengine wanateseka bila maji au chakula, ali mradi nimepata faida na utajiri wangu ubaki pale pale. Tunaogopa kuwasaidia wengine kwasababu tunadhani tutapungukiwa. Roho na akili yetu haina Amani usiku kucha kwasababu natafuta jinsi ya kutegemeza utajiri wangu, tumekamatwa sana na mali mpaka tunasahau nafsi ya Mungu katika maisha yetu. Tunakimbilia kwenye biashara kiasi chakushindwa hata kufanya ishara ya msalaba ili Mungu abariki mipango yetu. Mungu ni namba moja, mengine yote ni sifuri, tujitahidi kuitanguliza hii numba moja ili hizi sifuri zinazofuata nyuma yake zifanye yote yawe mengi, lakini ukitanguliza sifuri badala ya moja nadhani unajua utapata nini.
Kwa ufupi maisha yetu yatawaliwe na Mungu, chochote kamwe kisichukue nafasi ya Mungu. Mungu anapenda maadili yetu na thamani ya yote tulionayo yajengwe katika msingi wake yeye mwenyewe na hapo yataleta furaha na Amani kwetu. Mungu anajua mahitaji yetu hata kabla hatuja mwomba na anawapa wote kwa upendo wanao mtumainia.
Sala: Bwana naomba usinifanye maskini wala usinifanye tajiri mno, nishibishe kwa chakula ninacho hitaji nisije nikashiba mno nikakutukana nikasema “Mungu ni nani kwani?” au nisiwe maskini mno nikaiba nikalikashifu jina lako Mungu. Amina. (Hii ni sala ya kiasi) (Prayer of balance).
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni