SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU KRISTO
SOMO 1
Eze. 34:11-16
Bwana Mungu asema hivi: Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi, nitawatafuta kondoo zangu, na kuwaulizia. Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo zake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo zake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo zangu; nami nitawaokoa katika mahali yote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza. Nami nitawatoa katika watu wa mataifa, na kuwakusanya katika nchi zote, nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe; nami nitawalisha juu ya milima ya Israeli, kando ya mifereji ya maji; na katika mahali pote pa nchi panapokaliwa na watu. Nami nitawalisha malisho mema, na juu ya milima ya mahali yalipoinuka pa Israeli litakuwa zizi lao; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli. Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo zangu, nami nitawalaza, asema Bwana Mungu. Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.Eze. 34:11-16
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
(K) Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.
Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu;
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza. (K)
Sitapungukiwa na kitu;
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza. (K)
Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza
Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. (K)
Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. (K)
Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika. (K)
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika. (K)
Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)
SOMO 2
Rum. 5:5-11
Rum. 5:5-11
Pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Basi Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Yn. 10: 14
Yn. 10: 14
Aleluya, aleluya.
Mimi ndimi mchungaji mwema; asema Bwana; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
Aleluya.
Mimi ndimi mchungaji mwema; asema Bwana; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
Aleluya.
INJILI
Lk. 15: 3-7
Lk. 15: 3-7
Aliwaambia mfano huu, akisema, Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aenda akamtafute yule aliyepotea hata amwone? Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi. Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani yake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
[6/2, 22:07] Nyambane Maurice: “ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Juni, 3, 2016,
Juma la 9 la Mwaka
[6/2, 22:07] Nyambane Maurice: “ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Juni, 3, 2016,
Juma la 9 la Mwaka
Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
(Mwaka wa Huruma-siku ya kuombea utakatifu wa Mapadre)
(Mwaka wa Huruma-siku ya kuombea utakatifu wa Mapadre)
Ez 34: 11-16;
Zab 23: 1-6;
Rum 5: 5-11;
Lk 15: 3-7.
Zab 23: 1-6;
Rum 5: 5-11;
Lk 15: 3-7.
UPENDO WA MUNGU WA KUKOMBOA!
“Huu ni upendo si kwamba sisi tulimpenda Mungu kwanza bali yeye alitupenda sisi kwanza akamtuma mwanaye ulimwenguni kama sadaka kwaajili ya dhambi zetu” (1 Yn 4: 10). Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ni sherehe ya upendo wa ukombozi wa Mungu wetu. Mungu anayetupenda alimtoa mwanaye aje ulimwenguni kama sadaka kwaajili ya ukombozi wa Ulimwengu. Upendo huu unaoneshwa katika moyo wa mwana wa Mungu. Neno “moyo” linasimama kama upendo wa mtu. Na hivyo watu husema “Nakupenda kwa moyo wangu wote” na wakati tunapo sheherekea sikukuu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu kanisa linatuhimiza kutafakari juu ya upendo wa Mungu, upendo uliofunuliwa ndani ya mwili wa Mwanaye Yesu Kristo.
Ni Mungu aliyewachagua wa Israeli kuwa watu wake. Aliwabariki na akawachagua kuwa watu wake kati ya mataifa mengi. Si kwasababu walikuwa na nguvu kuliko wengine lakini kwasababu ya upendo wake. Hili ndilo Musa alilowafundisha watu wa Israeli. Anawakumbusha juu ya upendo wa Mungu juu yao. Upendo wa Mungu kwa watu wake hauna mwisho na hauna masharti. Aliwapenda watu wake pamoja na mapungufu yao na makosa yao. Na hata hivyo ubinadamu uliponaswa na dhambi alimtoa mwanaye wa pekee kwajili yetu. Kwahiyo tunapaswa kuuzoea nakuupenda upendo huu ili tuweze kuuelewa zaidi na kuwa watu wakweli wanotamani kuwa na Mungu daima. Ili tuweze kumpenda kwa moyo wetu wote na akili yetu zote.
Kwahiyo katika sikuu hii ya moyo Mtakatifu wa Yesu, tunamshukuru Mungu kwa upendo wake mkubwa kwetu anaotuonesha kila siku. Tuupende na kuushi upendo huu ndani mwetu ili tuweze kuwashirikisha na wengine.
Sala: Bwana, tuongoze kwenye mapendo yako ya ndani. Amin
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni