Baba Mtakatifu Francisku Alhamisi 11.08.16, alipata chakula chake cha mchana katika jengo la Mtakatifu Marta la ndani ya Vatican , akiwa na kundi la watu 21, wakiwa ni wakimbizi toka wa Syria wakiwa na watoto wao. Katika mlo huo, Papa kabla ya mlo huo, aliwapokea wageni wake upendo wa kibaba,akiwataka kila mmoja wao ajisikie nyumbani hata katika mazungumzo na barizi. Kabla ya mlo watoto walicheza na Papa.
Watoto walimzawadia Papa karatasi zenye michoro yao ya kitoto na Papa aliwaonyesha vitu mbalimbali vya kuchezea , madoli na zawadi nyingine. Wakimbizi hawa toka Syria, wanafadhiliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na walikuja Rome, tokea kambi ya wakimbizi ya Lesbos Ugriki ,wakiwa wameandamana na Papa Francisko, baada ya kuhitimisha ziara yake katika kisiwa cha Lesbos Ugriki tarehe 16 Aprili 2016. Wakimbizi hao walipanda ndege aliyokuwa akisafiria Papa kwenda na kurudi katika kambi ya Lesbos. Wakimbizi hao walikuwa ni kundi la kwanza kuja na ndege ya Papa. Kundi la pili lilifika Roma katikati ya Juni kwa Ombi lake Papa.
Alhamisi 11 Agosti, wakati i wa mlo huo wa mchana pamoja na Papa Francisko na wageni wake wa Syria, pia walikuwepo Naibu Katibu wa Jimbo la Papa , Askofu Mkuu Angelo Becciu; Profesa Andrea Riccardi, mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, na wanachama wengine kadhaa wa jumuiya hiyo; Pia Domenico Giani Kamanda wa kikosi cha usalama Vatican , na Maaskari wawili waliosaidia wahamiaji hao kuingia nchini Italia tokea Lesbos Ugriki .
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni