Mapema Jumatan 14 Septemba 2016, akiongoza Ibada ya Misa ndani ya Kanisa Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, Vatican, Baba Mtakatifu Francisko, alimtaja Marehemu Padre Jacques Hamel , kuwa ni shahidi wa imani na kwamba mashahidi wa imani ni wenye Heri. Marehemu PadreJacques Hamel , aliuawa wakati akiongoza Ibada Misa, tarehe 26 Julai na washambuliaji wa kigaidi.
Katika ibada hiyo aliyoiadhimisha kwa nia ya kumbukumbuka Marehemu Padre Hamel, Baba Mtakatifu Francisko katika homilia yake, alionyesha ukaribu wake kwa familia ya Marehamu na jamii nzima ya Rouen Ufaransa. Papa alisikitikia mauaji ya Padre huyo mpendwa, aliyeuwa na mikono ya vijana fedhuli wa Kifaransa , magaidi wenye asili ya kiarabu ,shambulio linalodaiwa kufanyika katika mtindo wa mauaji yanayofanywa na serikali ya Kiislamu ya Isis. Shambulio lililofanyika wakti wa maadhimishi ya Ibada ya Misa katika kanisa la Saint-Etienne-du-Rouvray.
Taarifa imetolewa kwamba,katika Ibada hii ya mapema Jumatano, iliyoongozwa na Papa Francisko katika Kanis adogo la Mtaktifu Marta kulikuwa na kundi la waamini wapatao 80 kutoka Jimbo la Rouen Ufaransa ambao walikuwa wameandamana na Askofu wao.
Katika homilía yake , Papa alirudia mara kwa mara kusema kwamba , mauaji ya kikatili ya Padre Hamel yanagusa moyo wake. Na kwamba maisha na kifo cha Padre Hamel , kimeongeza kuandika historia ya kifo na ushuhuda wa Kikristo, na hasa leo liturujia ikiadhimisha Siku Kuu ya Kutukuzwa kwa Msalaba. Papa anasema huu ni wakati ambamo Mama Kanisa anatafakari , jinsi Mwana wa Mungu", alivyo mwilishwa kama mwanadamu, na akawa mtii hadi kifo cha msalabani. Hivyo Yesu, ni shahidi wa kwanza wa upendo wa Mungu kwa binadamu. Hii ni siri ya Kristo, inayojionyesha katika historia yote ya kuuawa kwake, kama shahidi wa kwanza wa huruma ya Mungu kwa binadamu, ushuhuda unaoendelea kuonekana tangu karne ya kwanza hadi leo.
Baba Mtakatifu alieleza na kutaja sifa za Padre Hamel kuuawa kama shahidi wa Kristo madhabahuni, akitaja hisia zake zinazomfanya afikiri hivyo kwamba katikati ya wakati mgumu, Padre huyo, aliendelea kuwa mtu mpole, mtu mwema, mtu aliyependa kujenga udugu, na wala hakupoteza ujasiri wake katika kukemea waziwazi yaliyo kinyume na ubinadamu na aliwatamkia wazi wauaji wake akisema "Nenda zako, Shetani! '.
Papa alieleza na kuongeza kwamba , leo hii kuna Wakristo wengi wanaouawa , kuteswa, kufungwa jela na kuchinjwa kwa sababu, ya kukataa kukana imani yao kwa Yesu Kristo,kama ilivyotokea kaiak mauaji ya Padre Hamel , ambaye ni kati ya orodha ndefu ya Wakristo wanaokufa kama mashahidi. Watu anaoteswa na ukatili wa shetani , na hivyo sote mbele ya sura kama hiyo tunapaswa kusema , Nenda zako shetani.
Papa amemtaja Padre Hamel,kuwa mfano wa ujasiri huo. Mfano hai wenye kuleta matumaini kwa Wakristo wote kusonga mbele katika imani yao bila kuwa na hofu za kupambana na kifo. Papa alieleza na kutaja haja ya kuomba kupewa ujasiri huu wa kuwa shahidi! Ni lazima tumwomba Kristo atupatie ujasiri wa kuwa na upole, udugu, amani, hata kusema ukweli kwamba, : kuua kwa jina la Mungu ni ushetani .
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni