Wasiwasi juu ya hali ya nchi za Mashariki, kushutumu mabomu ya kemikali huko Siria ukiukwaji wa haki kimataifa,majaribio ya mashambuliz ya kigaidi dhidi ya wakristo wakiwa katika sala huko Misri na wito wa makubalino ya nchi za Israeli na Palestina, ni mambo msingi yaliyo jitokeza katika hotuba ya Askofu Mkuu
Bernardito Auza Katika hotuba yake huko New York.Askofu Mkuu Auza pia amebainisha juu ya ziara ya Baba Mtakatifu Francisko ya kwenda Misri inayo tarajiwa kufanyika tarehe 28 - 29 Aprili 2017 kuwa lengo ni kutaka kuwatangazia kuwa hakuna njia bora zaidi ya kuzuia chuki na kutumia nguvu kama siyo njia ya mazungumzo na makutano.Katika hotuba hiyo ametoa wito kwa wauza silaha kuchukua hatua kwa mujibu wa viwango vya kimataifa, na hata viongozi wa madhehebu ya kidini kujitokeza na kuwa wazi katika kuonesha umoja wa kila dini yoyote vitendo vya ugaidi kwa kutumia jina la Mungu,na pia kupinga vitendo vingine vinavyo kwenda kinyume haki ya binadamu,na msingi wa mwandamu yoyote , hasa haki ya maisha na uhuru wa dini.
Akiendelea na hotuba yake Askofu Mkuu Auza mawazo yake yamelenga pia uchache wa madhehebu ya kidini na makabila madogo ya nchi za Masahari ya Kati ambapo kihisotoria wameweza kuishi kwa amani maelfu ya miaka wengi wakiwa ni waislam, lakini leo hii madhehbu hayo madogo yako hatarini kutokana na itikadi kali ,ambapo malengo ni kuharibu utamaduni na urithi wa kihistoria. Kwa njia hiyo Askofu Mkuu anatoa wito kwa jumuiya zote za kimataifa kuongeza jitihada ili kuwakomboa watu na majanga wanayo kabiliana nayo kutokana na mauaji ya kinyama yanayofanywa na vikundi vya kigaidi. Mbele tishio la ukosefu wa usalama wa kuishi katika kanda za Mashariki ya kati, Askofu Mkuu Auza , ameisifu nchi ya Lebanon, walio chukua jukumu la kuwapokea mamilioni ya wakimbizi kutoka katika mipaka ya nchi hiyo. Kwa maana hiyo Vatican kwa mujibu wa masharti ya Baraza la Usalama,inatoa wito wa kusitisha silaha kwa kwa wale wanao tengeza na wale wanao fadhili utengenezaji wa silaha hizo ikiwa vyanzo vyake ni kutoka nje amesema.
Askofu Mkuu Auza pia katika hotuba yake aidha ametaja nchi mbili ya Israeli na Palestina zikiwa na mipaka ambayo imetambuliwa kwa ngazi ya Kimataifa ,amewataka wawe na mchakato wa makubaliano,kuwa na matashi mema ya ujasiri kwa lengo la kutaka Umoja; kwasababu vitendo vya kuendelea na vurugu na nguvu ndizo chanzo cha kuendeleza chuki na magawanyiko .Kwa njia hiyo anawaalika katika mazungumzo na mawelewano,akisema ndiyo mateshi mema ya Baba Mtakatifu Francisko mara nyingi nawakumbusha na kusali sana ili majeraha ya kina yanayotenganisha watu wa Israeli na Palestina yaweze kupona.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni