Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 7 Juni 2017 kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican amewaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuwa ni mashuhuda na vyombo vya huruma ya Mungu kwa jirani zao! Hata katika shida na mahangaiko mbali mbali, binadamu ataendelea kuwa ni mtoto mpendwa wa Mungu. Baba Mtakatifu anawataka waamini kujenga mahusiano mema na Kristo Yesu kwa
kukuza na kudumisha Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu. Mwezi Juni, unatolewa na Mama Kanisa kwa ajili ya Ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, uwasaidie waamini kusali kwa ajili ya kuombea amani na utulivu duniani, hasa kwa kuzingatia kwamba, kumekuwepo na wasi wasi na hofu ya vita na mashambulizi ya kigaidi sehemu mbali mbali za dunia!

Baba Mtakatifu anakaza kusema, Alhamisi, tarehe 8 Juni 2017, majira ya saa 7:00 mchana kwa saa za Ulaya, watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia, watasimama kwa dakika moja kwa ajili ya kuombea amani duniani. Hii ni kumbu kumbu ya mkutano uliofanyika kati ya Baba Mtakatifu Francisko, Marehemu Rais Peres Shimon wa Israel na Rais Mahmud AbbĂ s wa Palestina. Baba Mtakatifu anakaza kusema, bado kuna haja ya Wakristo, Wayahudi na Waislam kusali sana kwa ajili ya kuombea amani duniani! Sala kwa ajili ya amani huko Mashariki ni muhimu sana.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni