Baba Mtakatifu Francisko ameonesha huzuni mkubwa kwa kifo cha Kardinali Cormac Murphy-O'Connor, Askofu Mkuu mstaafu wa Westminster kilichotokea tarehe 1 Septemba. Katika Telegram yake kwa Askofu Mkuu wa sasa wa Jimbo Kuu la Westminster Kardinali Vincent Nichols, anamkubuka Askofu Mkuu mstaafu O’ Connor huduma yenye thamani aliyoitoa kwa ajili ya Kanisa la Uingereza na Galles, aidha kwa kujitoa kwa Kanisa zima katika kutangaza Injili na umakini wa maskini, juhudi zake za muda mrefu katika maendeleo ya safari ya kiekumeni na muungano wa madhehebu ya kidini. Anamkabidhi roho yake katika huruma ya Mungu Baba.
Pamoja na hayo taarifa kutoka katika Baraza la Maaskofu nchini Uingereza na Galles wanasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Cormac Murphy-O’Connor Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo la Westminster Uingereza, kilichotokea tarehe 1 Septemba 2017. Amekufa akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua kwa muda mrefu kwa ugonjwa wa saratani.Taarifa kutoka kwake Kardinali Vincent Nichols ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Westminster kwa niaba ya maaskofu wote anasema ameaga dunia akiwa amezungkwa na familia na marafiki zake;kwa njia hiyo, tumuombee ili aweze kupumzika kwa amani,pia tuwaombea wanafamilia wake, rafiki zake kutoka katika Jimbo na wote wanao omboleza kuondoka kwake. Taarifa za mazishi zitatolewa hapo baadaye.
Alizaliwa tarehe 24 Agosti 1932, akapata daraja la upadri mwaka 1956. Mwaka 1971 aliteuliwa kuwa gombera wa Chuo Kikuu cha kipapa cha Uingereza Mjini Roma na kuchaguliwa kuwa askofu wa Arundel na Brighton mwaka 1977. Tarehe 15 Februari 2000, Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua kuwa Askofu Mkuu wa Westminster na mwezi Novemba mwaka huo akachaguliwa kuwa Rais wa Baraza la maaskofu wa Uingereza na Galles. Tangu 2001-2006 alipewa majukumu ya kuwa Msaidizi wa Rais wa Baraza la maaskofu wa Ulaya (Ccee). Mwaka 2001 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Kardinali na tarehe 3 Aprili 2009 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akakubali maombi yake ya kustaafu baada ya kufikia muda wake, ndipo aliteuliwa askofu Mkuu wa Jimbo hilo ambaye kwa sasa ni Askofu Mkuu Vincent Nichols.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatica
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatica
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni