ASKofu
wa Jimbo Katoliki Mahenge Mhasham
Agipiti Ndorobo, amewataka wazazi kusisitiza sala za pamoja ndani ya familia
ili kujenga msingi wa imani ambayo inaanzia kwenye Familia
.
Askofu Ndorobo ameyasema hayo wakati wa
Ibada ya Misa Takatifu alipokuwa akitoa Sakramenti Takatifu ya kipaimara kwa
vijana 88 katika Parokia ya Mwenyeheri Anwarite Makuburi jijini Dar es Salaam.
Amesema kuipeleka Injili mbele
inawapasa waamini kwa pamoja kulingana na mazingira yao kuwajibika kuimarisha
imani Katoliki kwani si kazi ya mapadri na maaskofu tu kutangaza Injili.
Amesema kila mmoja ana karama zake
alizojaliwa na Roho Mtakatifu hivyo ni vyema akazitumia kujenga msingi imara wa
imani na kujenga taifa adilifu, lenye heshima na lenye watu wacha Mungu.Chanzo cha habari Na Philipo Josephati, Dar es Salaam TEC
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni