KATIKA safari ya
kueneza Injili kwa
watu wote hapa
duniani, Jimbo Kuu Katoliki Dodoma limepata
Parokia mpya ya
Pwaga iliyozinduliwa hivi
karibuni na Askofu
Mkuu wa Jimbo hilo Mhashamu Beatus Kinyaiya OFM-Capp.
Akizindua parokia
hiyo mpya hivi karibuni, Askofu Mkuu Kinyaiya OFM-Capp amesema kuwa
safari ya injili
ni ngumu na kuwa
si vyema wanadamu
kuipuuzia kwani ni
safari ya toba huku Kanisa likiwa ni
moyo wa muamini
popote pale na kuwa
pamoja na kuwa
parokia hiyo mpya
haina jengo kubwa lakini Kanisa ni
watu na ni popote
pale bila kujali ni wapi
wanasalia, la msingi ni kuwa
na imani kwa
Mungu.
“Mama Kanisa anasisitiza watu kusali kwa
moyo na nguvu
kubwa bila kujali
sala inafanyika wapi, mkristo anatakiwa kusalia mahali
popote kwani sala
ni Baraka na muamini
anapata nafasi ya
kuongea na Mungu
na si Kanisa. Parokia ya
Pwaga kwa uchanga
wake wa majengo
isiwe sababu ya
kuibeza bali na
itiwe nguvu na
waamini wake kwa
kusali kwa nguvu
na kuwa suala
la majengo makubwa na
mazuri yatakuja baadaye.” Amesema Askofu Kinyaiya.
Amesema parokia mpya
ya Pwaga imefunguliwa kutokana
na mahitaji ya
waamini kutaka huduma za
kiroho kufanyika karibu nao na
kuwa ombi hilo lilitolewa kwa
marehemu Askofu wa
pili wa Jimbo Kuu
Dodoma Mhashamu Joseph Isuja Shungu miaka
30 iliyopita yaani mwaka 1987.
“Kristo
hapatikani katika majengo
mazuri bali anapatikana
katika mioyo yenu, saline kwa nguvu
msitafute pa kusalia bali
pa kusalia pawe
popote ili mradi
mnasali kwa moyo
na Kristo atapatikana
hapo hapo mlipo, msifadhaike mioyoni
mwenu. Majengo mazuri na
makubwa yatakuja, ruhusuni Roho
Mtakatifu aingie mioyoni
mwenu atawaelekeza cha kufanya
huku mkijitoa kama
mlivyojitoa katika ujenzi
wa nyumba hii
ya mapadri.” Amesisitiza.
Amesema kwa sababu
parokia hiyo ya
Pwaga inaanza chini
yake, ni vyema
iwe kioo kwa
ajili ya kufundisha
watu kumuongokea Mungu
huku akiwaonya wana
kipaimara 26 aliowapa
sakramenti siku hiyo kulisikia neno
hilo na kulifuata.
Pamoja na kutangazwa
kwa parokia hiyo
mpya Askofu Mkuu
Beatus Kinyaiya OFM-Capp
amemtangaza Padri Nestory Ngunwa
kuwa paroko wa parokia hiyo mpya
na kuwa kwa
sasa atakuwa akikaa
parokiani Lumuma hadi hapo
nyumba mpya ya mapadri
hapo
Pwaga itakapomalizika.
Paroko wa Parokia hiyo
mpya, padri Ngunwa amesema
kuwa anamshukuru Mungu
kwa kumuona, na kwa
kutumwa na Askofu katika
parokia hiyo, ataifanya kazi
ya Bwana kwa
moyo wote.
Parokia hiyo mpya
ya Pwaga ina
vigango 12 ambavyo
ni Godegode, Mgoma, Kisisi,
Tambukareli, Wisuzaje, Idibulilo, Lufu, Kidenge, Gomhungile, Munguwi, Idaho na Maswala
.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni