Inahitaji ujasiri ili kufanya ufalme wa Mungu ukue, yaani wa kutupa mbegu ya aradali na kuchanganya chachu. Lakini mara nyingi wapo wachungaji wanaotaka kuhifadhi badala ya kupanda hiyo mbegu ili ikue. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati akitafakri Injili ya Mtakatifu (Luka 13,18-21) Siku tarehe 31 Oktoba 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Mjini Vatican.
Katika Injili ya siku Bwana Yesu anafananisha Ufalme wa Mungu kama mbegu ndogo ya aradali na chachu, kwa njia hiyo Baba Mtakatifu
anabainisha kwamba, mambo haya mawili japokuwa ni madogo, lakini ndani yake yana nguvu zaidi ya kukuza, ndiyo ilivyo hata ufalme wa Mungu maana una nguvu ndani yake.
Hata barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo iliyosomwa inaweka bayana mivutano ya maisha ya mateso, lakini inaoesha kwamba mateso hayo hayawezi fananishwa na utukufu tunao usubiri. Yote hayo ni mivutano kati ya mateso na utukufu,lakini katika mivutano hiyo bado kuna matatajio ya makubwa ya ufalme wa Mungu anathibitisha Baba Mtakatifu. Matarajio hayo siyo tu ya binadamu peke yake barua hiyo inasema, kwani ni viumbe vyote pia vinaugua pamoja navyo vina utungu. Baba Mtatifu anaongeza, lakini nguvu za ndani zinazotoa matumaini katika ukamilifu wa Ufalme wa Mungu ni Roho Mtakatifu.
Ni matumaini yanayotupeleka katika ukamilifu na kutoka katika kifungo cha: vizingiti, utumwa, ufisadi na kufikia utukufu, lakini hiyo inahitaji hija ya matumanini. Hata hivyo Baba Mtakatifu anasema matumaini ni zawadi ya Roho kwa maana roho Mtakatifu akiwa ndani mwetu, anatoa mambo mengi na makubwa, anakuokoa , anatoa uhuru na utukufu mkubwa. Na ndiyo maana Yesu anasema mbegu ya aradali japokuwa ni ndogo lakini ndani yake kuna nguvu zaidi ya kukuza jambo lisilofikirika.
Ndani mwetu kuna kazi ya uumbaji, kwa maana ni roho Mtakatifu anayetoa matumaini. Akifafanua zaidi anasema kuishi kwa matumaini ni kuachia nafasi nguvu ya Roho ili aweze kusaidia kukua kuelekea ukamilifu unaotungojea.
Kama ilivyo chachu kuchanganywa na unga, hata mbegu ya aradali lazima ipandwa ardhini, la sivyo nguvu yake ya ndani itabaki bila kuongezeka … ndivyo ufalme wa Mungu unavyokua ndani, lakini siyo kwa wapinzani wake.
Daima Kanisa limekuwa na ujasir wa kuchukua na kupanda, japokuwa, kuchukua na kupanda daima kunaleta hofu anaeleza. Hiyo ni kwasababu mara nyingi huonekana wachungaji wanaopenda kuhifadhi badala ya kuacha ufalme wa Mungu ukue. Lakini bila kuchukua mbegu na kupanda huwezi kukua bali itakaa ilivyo, hivyo ndivyo ufalme wa Mungu , hauwezi kukua, kwa njia hiyo, inahitajika ujasiri kufanya ufalme wa Mungu ukue… lazima kujikita katika kutupa mbegu na kuchanganya chachu anathibitisha Baba Mtakatifu Francisko.
Ole wao wanaohubiri Ufalme wa Mungu kwa kuwadanyanya wengine wakati wao hawataki kuchafua mikono yao. Hawa ni kama wale wanaotunza sanaa, wanapendelea mambo mazuri, lakini siyo ile ishara ya kutupa mbegu ili kwa nguvu iweze kuchanua, au kuchanganya chachu ili ukue. Huo ndiyo ujumbe wa Yesu na Mtakatifu Paulo mivutono ambayo inaanzia katika utumwa wa dhambi, ili uweze kuwa rahisi , na kukamilishwa na utukufu wa Mungu , na matumaini ni yale yanayojikita mbele bila kudanyanya kwasababu matumaini ni madogo sana kama ua mbegu ya aradali na kama chachu.
Baba Mtakatifu anaongeza kusema, matumani ni fadhila ya kinyenyekevu, ni huduma, lakini mahali ambapo kuna matumaini kuna roho Mtakatifu anayepeleka mbele Ufalme wa Mungu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni