0

Tarehe 6 Novemba 2017 Mchana katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican , Baba Mtakatifu amekutana na Bwana Kofi Annan aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1997 hadi 2006 akiongozana na wajumbe wengine wa Mashirika ya Kimataifa  yasiyo ya selikali “The Elders” Kati yao hata Bi Mary Robinson, aliyekuwa Rais  wa Jamhuri ya nchi ya Ireland mwaka1990-1997.

Hili ni Shirika lililoanzishwa  na Nelson Mandela miaka 10 iliyopita , kikundi kinacho jihusisha na kuhamasisha amani na haki za binadamu, ambacho kinaundwa na viongozi wa dunia na viongozi wa nchi walio angatuka madarakani, ndiyo maana jina lake ni “The Elders” maana yake wazee.....
Naamini sisi kwetu imekuwa muhimu kuja hapa kwasababu tuna mambo muhimu yanayotuunganisha  pamoja na Baba Mtakatifu na tumetaka kukutana naye ili kufikiria jinsi gani tunaweza kufanya kazi kwa pamoja na kutia juhudi zetu zote katika mambo muhimu. Ni maneno Bwana Kofi Annan katika Mahojiano na mwandishi wa habari wa Radio Vatican mara baada ya mkutano na Baba Mtakatifu Francisko.

Bwana Kofi Annan anasema, katika mkutano wao na Baba Mtakatifu wamegusia mada ya wahamiaji na wakimbizi, silaha za kinyuklia, mada ambayo Vatican imeandaa pia Mkutano wake utakaoanza hivi Ijumaa ijayo. Wamezungumzia juu ya mani na kutafakari kwa kina juu ya michakato inayoweza kufanywa ili  kuisha kwa migogoro mingi duniani na hata hivyo akataja kuwa  Bi “Mary Robinson anaweza kueleza mazungumzo juu ya wanawake na umuhimu wa kuwapa sauti wanawake, heshima na nafasi waliyo nayo katika jamii.  Na mwisho amesema, Bwana Annan kuwa,  ni matumaini yake ikawa ndiyo mojawapo ya  mwanzo wa mikutano mingi ambayo wataweza kuifanya na Baba Mtakatifu.

Kwa maana hiyo hata  Bi Mary Robinson katika maelezo ya mkutano na Baba Mtakatifu  ametoa sifa nyingi kwa ajili ya nafasi ya Baba Mtakatifu, kwa kazi anazozifanya hasa kwa juhudi ambazo anatoa sauti kwa ajili ya wale wasio kuwa na sauti, walio baguliwa au kukabiliana na mambo nyeti na magumu kama yanayo husu  suala la nchi ya Venezuela, kwa mantiki ya Bara la Amerika ya Kusini, Congo na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo kwa namna ya pekee ni hali halisi anayojikita nayo.
Bi Robinson pia ameelezea juu ya kupokelewa vema na Baba Mtakatifu,ambapo yeye binafsi  amebaki na mshangao kwa ukarimu wake, kwa maana wameweza kucheka na kutaniana kama vile  ni mmojawapo wa kikundi chao, anasema kweli amejisikia kuwa mmoja kati yao na wametambua walivyo na mambo mengi ya pamoja yanayofanana na yenye thamani,mapendekezo ya maadili na matatizo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatica

Chapisha Maoni

 
Top