HISTORIA FUPI YA IBADA YA
ROZARI.
UTANGULIZI
Katika Kalenda ya Kanisa
Katoliki, huwa mwezi wa tano na mwezi wa kumi ni miezi ambayo imewekwa kwa
ajili ya Bikira Maria na Mama Kanisa. Hivyo hiyo miezi huwa inasaliwa rozari
kwa heshima na maombezi ya Bikira Maria. Wengi waweza kujiuliza kuwa ni kwa
nini ifanyike miezi hiyo? Yafuatayo ni majibu:
Mwezi wa tano umewekwa kwa
heshima ya Bikira Maria kutokana na nini kilitokea katika historia hapo nyuma.
Mnamo Karne ya 16 mwezi watano kwa miaka yote ulikuwa ni mwezi ambao sikukuu
nyingi za kiserikali ndo zilikuwa zikifanyika.
Kanisa kwa kutambua hilo
nalo likaidhinisha pia mwezi wa tano uwe ni mwezi wa Rozari, na kwa makusudi
zaidi Kanisa lililenga kuwa sherehe hizo ziendane na taratibu za wakristu. Ni
kwa msingi huo sherehe hizo ziliendana na mwezi wa rozari na kutokea hapo
ikahidhinishwa kuwa mwezi wa tano wa mwaka ni mwezi wa Bikira Maria.
Pia mwezi wa kumi (October)
ni mwezi wa Bikira Maria na pia ni mwezi wa Kusali Rozari kutokana na historia
ya hapo nyuma pia. Ilikuwa kwamba baada ya ushindi wakristo walioupata katika
vita baina yao na yule aliyeitwa Lepanto mnamo 7 October, 1571, Papa wa wakati
ule Papa Pius V aliufanya huo ushindi kuwa ulitokana na maombezi ya Bikira
Maria, na alisema kuwa rozari ni silaha kubwa hata kuliko silaha kubwa za
kivita. Ni Kwa msingi huu tunaona kuanzia hapo mwezi wa kumi ukawa mwezi
uliotengwa na Mama Kanisa kumuenzi Mama Bikira Maria, na pia ukaitwa mwezi wa
Rozari.
Fr. Revocatus Paul anaendelea
kuelezea historia ya Ibada ya Rozari:
Historia yenyewe
Ni kwamba sala ya Rozari inasemekana kuanzishwa na Mt. Dominico
aliyezaliwa mnamo mwaka 1170 na kufariki mwaka 1221 na hiyo sala Mt. Dominico
aliipata kwa njia ya ufunuo ambapo Bikira Maria alimtokea na kumwamuru awe
anasali rozari.
Bikira Maria alimwamuru mtakatifu Dominico kusali rozari kwa
kipindi hicho iwe kama silaha yake ili kupambana na uzushi uliokuwa umeibuka ukipingana
na mafundisho ya Kanisa, na huo uzushi uliitwa ‘ Albigensia’ hili ni kundi
lilokuwa na imani kuwa Duniani kuna nguvu mbili zenye uwiano sawa lakini
hupingana na kupigana moja baada ya nyingine, nazo nguvu hizo ni Mungu na
Shetani.
Hivyo hawa waliamini kabisa kuwa Mungu na Shetani wana nguvu
sawa ( Dualistic ) waliamini pia kuwa dunia hii imejaa uovu kwa kuwa iliumbwa
na mwovu. Ni kwa msingi huu Kanisa liliamua kupambana na hawa wazushi ambao pia
walionekana kupotosha mafundisho ya Kanisa. Ndipo tunaona Bikira Maria
anamtokea Mtakatifu Dominico na kumwambia asali rozari ili kupambana na
mafundisho hayo ya kizushi. Ni Papa Pio V ambaye mnamo mwaka 1569 alihidhinisha
rasmi kusali rozari kwa kanisa nzima na kuhidhinisha rozari iwe jinsi
tunavyoiona sasa.
Katika zile zama za kati, watawa wamonaki walizoea kusali zaburi
150, na kwa upande wa waumini walei ambao kwa kipindi hicho hawakujua kusoma
zaburi iliwabidi wasali sala ya Baba yetu mara 150 baadala ya zaburi 150 na
hizo baba yetu walizisali kwa kuhesabu punje 150 zilizokuwa zimefungwa kwenye
kamba ndefu ambayo kwa lugha ya kitaalamu iliitwa “ Corona” au kwa Kiingereza “
Crown” kadiri ibada kwa Bikira Maria ilivyoendelea kushamiri mnamo Karne ya 12,
sala kwa Bikira Maria ilianzishwa na hivyo kuanza kusali salamu maria 150
baadala ya baba yetu 150.
Salamu Maria 150 hapo baadaye zilikuja
kugawanywa katika makundi/ mafungu na Mtawa mdominica aliyeitwa Henry Kalkar (
1328-1408), ambapo kila tendo la rozari lilikuwa na mafungu 50 ya salamu Maria
ambapo pia kila fungu liligusia maisha ya Bikira Maria na Yesu katika historia
ya wokovu wetu.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni