0
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki Mwanza Yuda Thadei Ruwaichi amekemea vikali ndoa za jinsia moja na kusema sasa ni wakati muafaka kwa jamii kuzikomesha.

Amekemea ndoa hizo jijini Mwanzakatika misa takatifu ya azimisho la sikukuu ya wakina baba iliyofanyika katika parokia ya Kawekamo jijini humo.
Askofu Ruwaichi amesema hakuna familia yoyote takatifu inayoweza kutengenezwa na watu wawili wa jinsia moja walioamua kuishi pamoja kindoa.
Amesema ndoa takatifu ni ile ya mme na mke kuoana na kupata Baraka zote za Mwenyezi Mungu.
“Watu wanamkosoa Mwenyezi Mungu kwa kuamua kuoana mme kwa mme ama mke kwa mke na kuamua kuasili watoto kitu ambacho hakikubaliki katika dini yoyote”Amekemea Askofu Ruwaichi.
Amelaumu tabia za baadhi ya mataifa makubwa yaliyoendelea kuyashauri mataifa madogo yanayoendelea kukubaliana na tabia hizi alizoziita”chafu” kwa kisingizio cha misaada na haki za binadamu.
“Mwenyezi Mungu alikuwa na maana kubwa kuweka ndoa takatifu ,kutoa zawadi,tunu,furaha,upendo na Baraka kwa mke na mme walioamua kuishi pamoja na kujenga familia,sasa iweje leo mwanadamu apinge hilo?”Amehoji
Amewataka wanafamilia(mke na mme)kuishi kwa amani,furaha,upendo na imani kwa Mwenyezi Mungu ndani ya familia hasa kwa kuzingatia kuwa muunganiko huo ni kanisa la nyumbani.
Sambamba na kemeo hilo,Askofu mkuu amewataka mapadri wote wa Jimbo kuu Mwanza kuitafsiri,kuifundisha na kuisambaza hati fundishi(furaha ya upendo)katika kila Jumuiya ili iziboreshe familia.
Hati hiyo inatoka kwa Baba Mtakatifu Papa Francisko lengo lake likiwa kuziimarisha familia takatifu.

Bernard James,Mwanza


Chapisha Maoni

 
Top