Askofu
John Ndimbo kutoka Sektretarieti ya huduma za kijamii Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania katika mahojiano maalum na Radio Vatican anabainisha baadhi
ya changamoto zinazoikumba sekta ya elimu nchini Tanzania na jinsi ambavyo
Kanisa linajitahidi kuboresha sekta hii katika taasisi za elimu zinazomilikiwa
na kuendeshwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kuanzia shule za awali,
msingi, sekondari, vyuo vikuu pamoja na taasisi za elimu ya juu.
Idara
ya elimu kitengo cha huduma za kijamii cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
kimeamua kuunda kitengo cha ukaguzi kitakachofanya tathmini kuhusu: kiwango na
ubora wa elimu inayotolewa kwa watanzania na Kanisa Katoliki, tayari kutoa
ushauri kwa wadau mbali mbali ili kurekebisha au kuboresha zaidi pale
inapoonekana kwamba, inafaa.
Idara
ya elimu kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Mtakatifu Augostino cha Tanzania,
SAUT kimekuwa kikiendesha semina za mara kwa mara kwa wakuu wa shule, taasisi
za elimu ya juu na vyuo vikuu vinavyoendeshwa na Kanisa Katoliki nchini
Tanzania, ili kuwapatia sera na mikakati ya stadi za uendeshaji wa taasisi za
elimu zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania. Kanisa linatambua kwamba, hii
ni huduma muhimu sana katika jamii inayopaswa kutolewa pasi na ubaguzi wa imani
au itikadi ya mtu. Kanisa linashirikiana kwa karibu sana na Serikali katika mchakato
wa maboresho ya elimu kadiri ya miongozo, taratibu na kanuni zinazotolewa na
Serikali chini ya mwamvuli wa wadau wa sekta binafsi ya elimu nchini Tanzania.
Majimbo
mbali mbali yanaendelea kuboresha miundo ya sekta ya elimu ili kukidhi ubora na
viwango vinavyotolewa na Idara ya elimu anasema Askofu Ndimbo. Jambo linalotia
moyo na faraja kuu ni kuona jinsi ambavyo Maaskofu wanaendelea kuwekeza katika
majiundo makini ya rasilimali watu kwa kuwasomesha Wakleri na Watawa tayari
kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uongozi kwa taasisi za elimu
zinazomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki Tanzania. Cheche za mafanikio
haya zinaanza kujionesha nchini Tanzania.
Na
Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa
ya Kiswahili ya Radio Vatican
Askofu John Ndimbo kutoka Sektretarieti ya huduma za kijamii Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika mahojiano maalum na Radio Vatican anabainisha baadhi ya changamoto zinazoikumba sekta ya elimu nchini Tanzania na jinsi ambavyo Kanisa linajitahidi kuboresha sekta hii katika taasisi za elimu zinazomilikiwa na kuendeshwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kuanzia shule za awali, msingi, sekondari, vyuo vikuu pamoja na taasisi za elimu ya juu.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni