0

MBINU ZA UIMBAJI

Nazipongeza kwaya zetu nyingi kwa kujitahidi kufanya vizuri kila siku.
Jambo ambalo walimu wengi wa kwaya wanalisahau kulifanya katika kwaya zao ni kuwafundisha wanakwaya mbinu (techniques) za uimbaji. Mara nyingi kisingizio kimekuwa ni uandaaji wa Liturjia ya Jumapili (hata zile kwaya zilizo na umri mkubwa? Jamani!)
Mfano rahisi ni huu:


Waimbaji wengi wa kike wanashindwa kutamka vizuri maneno notes zinapofikia na kuzidi D ya pili toka middle C; hili ni tatizo kwa kwaya zote nilizowahi kuzisikia hapa Tz; je, tumeridhika na kuliacha tatizo hilo lituonee? Hilo ni moja tu; yako mengine mengi Tunafanya nini basi? Tunachopaswa kufanya ni kutenga siku moja ya mafunzo ya mbinu za uimbaji kwa waimbaji wetu ili waweze kuimba vizuri zaidi na sio kuwajaza nyimbo lukuki ambazo zinaimbwa vile vile kila siku!
Ili suala la mafunzo ya mbinu za uimbaji lifanikiwe, walimu wanatakiwa kwanza KUWEZA KUIMBA VIZURI WENYEWE ili wawe mfano kwa waimbaji wao. Baada ya hapo ndipo tunaweza kuwapa waimbaji mbinu hizo kwa usahihi. Kuna websites na videos kwenye YouTube etc. zinazofundisha mbinu za uimbaji; tuzitafute. Vile vile, tusisite kuwakaribisha walimu wenzetu waliotuzidi katika hilo ili kwaya yetu ifaidike.
Pia, tuwaencourage akina dada na akina mama kujifunza muziki na kujiongeza ili tupate walimu wengi wa kike. Tatizo la uimbaji katika sauti za kike kwa asilimia kubwa husababishwa na ukweli kwamba walimu wanaowafundisha ni wanaume! Kutakuwa na mabadiliko makubwa endapo Soprano na Alto wakafundishwa na mwalimu wa kike; translation ya sauti haitahitajika!
Zaidi ya hapo, walimu wawe na plan ya mafunzo ambayo itajulikana kwa kamati ya ufundi; hii itasaidia hata kama mwalimu hayuko kujua nini kinapaswa kufanyika siku ile ili akipatikana mwalimu wa kusaidia ajue nini afanye.
Nina uhakika hili likifanyika matunda yake tutayafurahia kwa muda mrefu sana. Sijasema kwamba ni rahisi; hili ni jambo lenye changamoto nyingi mno; wanakwaya wengine wataligomea, na si ajabu hata viongozi wengine wa kwaya watalipuuza n.k. Then again, hakuna kizuri kisichotokewa jasho (na nyakati nyingine hata damu)
Nawatakieni utume mwema!


Chapisha Maoni

 
Top