Ni
wajibu wa wabatizwa wote kumtangaza Kristo kila mahali
Baba
Mtakatifu Francisko, Jumapili akisali sala ya Malkia wa Mbingu,Jumapili
ya saba ya kipindi cha Pasaka, alihimiza Wakristo kumhubiri Kristo, kila mahali
duniani bila woga. Himizo hilo alilitoa mbele ya maelfu ya mahujaji na
wageni waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu
Petro , Jumapili hii ambayo pia Mama Kanisa alikuwa akiadhimisha Sikukuu ya
Kupaa Rabbi, na Siku ya Mama wote .
Akitoa
hotuba fupi juu ya siku kuu ya Kupaa Rabbi , Papa alisema, "awali
kabla ya kuwaacha marafiki zake , Yesu alifanya rejea katika kifo na ufufuko
wake , akisema ninyi ni mashahidi wangu. Na kumbe Yesu anawataja mitume wake
waliokuwa mashahidi wakati wa mateso kifo na ufufuko wake pia wanakuwa
mashahidi wake wakati wa kupaaa kwake Kristo"
Baba
Mtakatifu aliendelea kusema, "Kwa kweli, baada ya kuona Bwana wao anapaaa
mbinguni, wafuasi walirudi mjini, wakishuhudia kwa furaha na guvu zote
kama mashahidi, walivyomwona Yesu akipaa mbinguni. Kwa furaha walitangaza
hilo kwa kwa kila mtu, na juu ya maisha mapya yanayoletwa na Kristo
Mfufuka,na katika jina lake, walihubiri katika mataifa yote, toba
na msamaha wa dhambi.
Baba
Mtakatifu aliendelea kusema, walikuwa mashahidi si kwa maneno tu lakini pia kwa
matendo katika maisha ya kila siku.Na hivyo Papa akatoa wito kwa
wabatizwa wote wa Kristo akisema, ni kutoa ushuhuda kila siku, kama
inavyotangazwa na Makanisa kila Jumapili na kuendelea kwa wiki nzima, katika
nyumba zetu, ofisi zetu, shule zetu, kukusanywa kwetu maeneo na kumbi za
burudani, hospitali zetu, magereza, na nyumba kwa ajili ya wazee, katika maeneo
inaishi wahamiaji, nje na ndani ya miji. Ni lazima kupeleka ushuhuda
huu kila wiki kwamba Yesu kapaa mbinguni , lakini yu pamoja nasi.
Kristo ni hai!
Pia
Papa wakati huo wa sala la Malkia wa Mbingu , aliwakumbuka Wamama wote
duniani, kwa kuwa pia ilikuwa ni Siku ya Dunia ya kuwaenzi wamama wote,
wenye watoto hata wasiojaliwa watoto. Alisema" katika siku hii, kwa
heshima na taadhima , tunawaenzi kwa upendo mkuu, wamama wote walio kati yetu
na hata waliotutangulia mbele ya Uso wa Bwana. Kwao wote tunawakabidhi kwa
Mama Maria Mama wa Yesu". Kwa ajili yao wote Papa
aliwashukuru kwa kuipokea dhamana hii ya kuwa mama waliyopewa na
Mungu na kwa ajili yao alisali ya Salaam Maria.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni