Kusema hiki na kutenda kinyume chake huo si ukatoliki. Ni lazima kuchagua moja au kuwa mtu wa dini au bila dini. Ni mahubiri ya Papa Francisko wakati akiongoza Ibada ya Misa mapema Alhamis katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta la mjini Vatican. Papa aliangalisha katika madhara yanayosababishwa na watu wa Kanisa na hasa Watumishi wa Kanisa wanaofanya kinyume na kile wanachokisema. Hivyo Papa amehimiza kuwa huru kujinasua na yale yanayoonekana kama masharti au sheria zinazokwamishwa huduma miongoni mwa jamii.
Homilia ya Baba Mtakatifu Francisko ililenga katika somo la Injili ambamo Yesu alihimiza uhalisia wa mafundisho ya Kikristo, kwamba yamejikita katika msingi wa utendaji wa haki zaidi ya sheria zilizokuwa zikitangazwa na waandishi na Mafarisayo. Baba Mtakatifu alisema,watu walikuwa wamechoshwa kidogo na mafundisho ya Mafarisayo kwa kuwa zilikuwa ni sheria nzito ambazo wao wenyewe mafarisayo walishindwa kuziishi. Hivyo Yesu aliwataka watu kutenda kwa busara na hekima wakati wakitimiza sheria hizo. Ili watu wapate kuelezwa zaidi anachokisema, Yesu aliwapa mfano wa Amri ya kwanza:Kumpenda Mungu na kumpenda jirani , akiongeza kwamba, hata kuendelea kumkasirikia ndugu yako ni kutenda kosa.Ni veyma kufanya haraka kujipatanisha nae, kabla ya kwenda kushiriki katika Ibada, kumtolea Mungu sadaka ya misa. Papa alifaanua kwamba, kumkasirikia ndugu ni kosa kwa sababu hudhoofisha utakaso wa roho.
Papa alieleza na kuonya kwa jinsi watu walivyokuwa na mazoea ya kutumia maneno mazito mazito na misamiati kutukana wengine . Alisema hili ni dhambi , tena ni dhambi ya kuua wengine kwa sababu ni sawa na kofi katika nafsi ya wengine, matusi ni kofi linalo dharirisha heshima na utu wake. Aliongeza kuwa pia maneno ya kejeli huongeza uchungu moyoni.
Na kisha Papa alitazama kashifa zinazofanywa na wanakanisa, wanaokuwa kama mafarisayo wanaobebesha wengine sheria nyingi zito za kanisa lakini wao hawawezi kujiishi. Yesu aliwaambia Mafarisayo ninyi mliwadhuru na kuwaua manabii walio waudhi, watu waliokuwa wakitengeza njia ya mema mapya katika jamii.. Yesu, katika hili anatoa wito kwa watu wake, kushika yanayohubiriwa na kusonga mbele katika neno lake. . .na wakati huo huo, Kristo alionya kuhusu madhara yanayosababishwa na watu wa Mungu na Wakristo ambao hawafuati mafundisho yao wenyewe.
Papa alizitazama hali halisi za maisha ya leo akisema, ni mara ngapi tunayasikia mambo haya katika kanisa! Padre au askofu na hata kwamba Papa kutuambia ni lazima kufanya hivyo kwa njia hii!' lakini wao wanafanya kinyume. Hii ni kashfa kubwa yenye kurejeruhi mioyo ya watu na kuzuia watu wa Mungu kukua katika imani na kusonga mbele. Imani ya viongozi hao ni bure kama ilivyokuwa kwa mafarisayo na waandishi waliokemewa na Yesu kwa kuwatendea watu na hata kuwaua manabii, walivyowaudhi manabii.
Papa alieleza na kusema, hivyo kumbe kuwa mfuasi wa kanisa hakuna cha utendaji wa nusunusu lakini ni kutenda kwa ukarimu na utakatifu wote, kama Yesu anavyotaka. Daima ni kujifunua wazi katika utumishi kwa ajili ya wote. Yesu anakataza unafiki , unafiki katika ibada na unafiki katika masifu na unafiki katika maisha. Papa Francisko alikeme tabia ya unafiki wa kujifanya unampenda ndugu yako au jirani kumbe ndani ya roho yako unatukuta kwa hasira na matusi juu yake.
Aliongeza, Yesu anaonya, ni lazima kujiepusha na tabia ya marubano na vita kati yetu. Ni lazima kufanya kila bidii kuhakikisha tunaishi kwa amani na ndugu zetu na majirani zetu. Alimwomba Bwana Yesu kutufundisha, kwanza, kuweza kuyapokea matatizo na shida za wengine, na kisha kuwa na uwezo wa kuabudu na kumtukuza Mungu. Kutufundisha mapatano kati yetu; na pia, atufundishe kukubali kwa uhakika kwamba tunaweza kufanya hivyo.
Chanzo cha Habari ni RadioVatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni