Ijumaa hii Juni 10, 2016, ujumbe kutoka Usharika wa Reformed Churches”duniani, ukiongozwa na Rais wa Usharika huo Mchungaji Jerry Pillay na Katibu Mkuu Mchungaji Chris Ferguson, umepokewa na Papa Francisko mjini Vatican na kuwa na mazungumzo ya pamoja yaliyolenga kuimarisha zaidi uhusiano kati ya Makanisa.
Papa akizungumza na ujumbe huo, kati ya mengine ameutaja ugeni huo, kuwa ni hatua moja mbele katika juhudi za kiekumene, na pia ni baraka na matumaini katika njia ya kutembea pamoja kwenye jitihada zinazotafuta kuwa na umoja kamili kwa mujibu wa Sala ya Bwana "ili wote ulionipa wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja”(Yn 17:21 ).
Papa katika hotuba yake kwa ujumbe huu wa Makanisa ya Reformed Churches, imesisitiza kama jambo la kidharura , kukuza uwezo wa kiekumeni, katika kazi za uinjilishaji na huduma ya kiroho, sadaka ya uponyaji na ukombozi unaopatikana katika kanisa la Kristo.
Papa Francisko amekubusha pia kupita kwa ipindi cha zaidi ya miaka kumi tangu ujumbe kutoka ushariki Reformed Churches, ulipofanya ziara yake Vatican na kupokewa na Mstaafu Benedict XVI, umoja unaoonyesha mafanikio kuelekea ujenzi wa umoja wa Wakristo, na hivyo inakuwa ni chanzo cha faraja kwa wengi wanaotembea katika njia ya ekumeni.
Papa ameendelea kumshukuru Mungu kwa undugu uliopo , kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyoandika, si matokeo ya moyo wa hisani au roho ya kifamilia isiyoeleweka , lakini inatokana na utambuzi wa mzizi wa umoja unaochipushwa na Ubatizo mmoja na wajibu wa kumtukuza Mungu katika kazi yake (cf. Ut Unum Sint, 42). Aliendelea kusema, katika ushirika huu wa kiroho, Wakatoliki na madhehebu mengine ya Kikristo , wanajitahidi kuwa pamoja, katika njia hii y aumoja kwa ajili ya kufanikisha kazi za Bwana.
Kwa mtazamo huo, Papa amesisitiza kama jambo la kidharura, kufanikisha majadiliano ya kiteolojia, yanayolenga kuondoa utamaduni wa kutoelewana katika mafundisho kati ya Wakristo, pia uwezekano wa kukuza zaidi ushirikiano kwa ajili ya uinjilishaji na huduma.
Baba Mtakatifu Francisko alieleza na kurudia kutoa shukurani zake za dhati kwa ziara yao na majitoleo yao katika huduma kwa Injili. Na pia alionyesha tumaini lake kwamba kukutana kwao , inekuwa ni ishara madhubuti katika safari ya pamoja kuelekea umoja kamili. Anasema kuwa huenda tukio hili, likawatia moyo zaidi wajumbe wote wa tume inayohusika na marekebisho yanayoendelea kufanywa kwa pamoja kwa ajili ya kufanikisha matumaini na faraja zaidi kwa waamini wa Kanisa.
Ujumbe kutoka ushariki wa Maknisa ya Reformed Churrches uliomtembelea Papa Francisko ni pamoja na Rais wa Ushariki Mchungaji. Jerry Pillay, Katibu wa Ushariki Mchungaji Chris Ferguson, akiwepo pia Mchungaji Dora Arce Valentin, Katibu mtendaji kwa ajili ya haki; na Dk. Aruna Gnanadason, mshauri kwa teolojia na Gabriela Mulder, rais wa Ushariki wa Presbyterian na Amerika ya Kusini na Caribbean; Mchungaji Eugene Bernardini, msimamizi wa Kanisa la Valdese, na Phil Tanis, ambaye ni Katibu Mtendaji kwa ajili ya mawasiliano katika Ushirika huo.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni