Baba Mtakatifu Francisko amewataka Wakristo wote :Kufuata na kuziishi Heri Nane zilizotangwa na Yesu, kama dira ya maisha ya haki kwa Wakristo. Papa alitoa mwaliko huo wakati wa Ibada ya Misa , mapema Asubuhi Jumatatu hii, katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta la hapa Vatican. Mwaliko wa Papa, unahimiza maisha adilifu yaliyo kinyume na moyo wa kuabudu utajiri, ubatili na ubinafsi.
Papa alitoa wito kwa kurejea mafundisho ya Yesu ya Mlimani ambako alitangaza tabia nane za maisha adilifu kama mwongozo wa maisha ya imani kwa Mungu na utendaji wa haki, mwogozo unaojulikana kama Heri Nane . Papa alionya kupuuzia yaliyomo katika mwongozo huo ni mwanzo wa kupoteza mwelekeo wa maisha na hivyo kuanguka katika mambo yaliyo kinyume na Ukristo, na kuwa na roho yenye kuabudu fedha, ubatili na ubinafsi, nanbio yanayoleta furaha bandia na kupuuza wengine.
Papa Francisko amesema,Mafundisho mapya ya Yesu si kama yalifuta sheria za kale zilizokuwapo lakini yalikamilsha sheria hiz katika ukamilifu wake. Na kwamba sheria hizi mpya za Bwana ni kwa dira ya kutuongoza katika njia yetu ya maisha adilifu ya Kikristo, ambamo kwayo tunaona kuwa ni njia ya kuendelea kutenda haki wakati tukisonga mbele na maisha kama Wakristo.
Baba Mtakatifu Francisko alieleza na kuwataka Wakristo wote , kujinasua na moyo wa kupenda mali, ubinafsi na ubatili, kwa kuwa Yesu alikwisha onya”ole wenu ninyi mlio na mali , kwa kuwa faraja yenu mmekwisha ipata. Katika hili Papa asema si vibaya mtu kuwa na tajiri, lakini anachoonya Yesu ni mtu kushikamana na utajiri na kumsahau Mungu. Kuifanya mali kuwa ndiyo kitu cha kwanza katika maisha badala ya kumtanguliza Mungu katika yote. Kinachokatazwa na kuifanya mali kuwa miungu na kuibudu kwa katika maana kwamba, akili yote na nafasi ya kwanza katika fikira inakuwa juu ya mali hiyo. Mali kupewa nafasi ya kwanza katika maisha.
Papa aliendelea kufafanua kwamba, Yesu alikamilisha sheria hizi kama mwongozo wa kupambana na ubaya katika maisha. Sheria hizo zinatukumbusha kutojenga moyo wa majivuno na ubinafsi wa kujiona tumejikamilisha katika kila jambo, kama ilivyokuwa kwa Mfarisayo aliyesali, makushukuru kwa kuwa mimi si kama yule, nataoa sadaka zote, nasaidia maskini, naongea vizuri na kila mmoja ananifahamu mimi kwamba ni mtu wa haki kuliko wote. Papa majigambo kama hayo ni upofu wa moyo. Na hat aleo hii kuna wenye tabia kama hiyo ya majigambo, mimi ni Mkatoliki safi , si kama jirani yule, naenda Kanisa kila siku, nafanya hili, nafanya lile, huko ni kujiridhisha mwenyewe, hicho ni kicheko bandia moyoni, kwani haijulikani kesho itakuwaje.
Papa Francisko alieleza na kuomba kila mmoja atafakari kwa makini mafundisho hayo ya Yesu kwa wafuasi wake, ikiwemo Heri wenye upole maana hao watairithi Nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki maana hao watashibishwa… Yesu anasema, 'Mjifunze kutoka kwangu, maana mimi ni mpole wa moyo. Kumbe upole ni njia inayotuleta karibu sana na Yesu. .Papa alieleza na kuomba msaada wa Roho Mtakatifu utusadie kuuelewa kwa kina, ukuu wa Mungu, na Ibada.
Chanzo cha habari n Radio Vatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni