Pengine
umewahi kuulizwa swali hili au umewahi kujiuliza: hapa ni maelezo
yatayokusaidia kuelewa sababu (japo sio zote) na uhalali wa jambo hilo.
Hapa
tunaongozwa na maneno ya Bwana Yesu mwenyewe alipotoa amri hiyo kwa mitume wake
akisema;
"Pokeeni Roho Mtakatifu.wowote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa na wowote mtakaowafungiwa dhambi wamefungiwa"(Yohane 20:22-23).
"Pokeeni Roho Mtakatifu.wowote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa na wowote mtakaowafungiwa dhambi wamefungiwa"(Yohane 20:22-23).
Na
huo ndio utaratibu wetu tangu mwanzo wa kanisa wa mitume.
"Ungameni
dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa"(Yakobo 5:16a)
Ni
miongoni mwa maagizo msingi kabisa ambayo hatuna mamlaka kuyabadili labda Yesu
mwenyewe aliyeagiza hivyo aje mwenyewe kuyabadilisha.
Mungu
anayesamehe dhambi ndiye aliyechagua njia ya kutoa msamaha huo,sisi tu nani
tumpangie njia ya kutoa msamaha huo na kujipangia njia zetu?je tunamfundisha
Mungu kazi?
Inashangaza
siku hizi kusikia kwamba hata baadhi ya wakatoliki wameanguka katika mtego huu
wa kutaka kubadilisha agizo hili la Yesu na inashangaza ni kwanini wanataka
kurahisisha mambo kiasi hicho.
Mungu
hafanyi kazi zake hewani bali huzifanya kupitia kwa watu wake.
Tunapoomba
msamaha tunategemea kusikia maneno kama vile "nimekusamehe",hutaka
kuamini kwamba mtu akinyamaza au akiongea kimoyomoyo basi amekusamehe.
Yesu
kwa kujua umuhimu na kazi ya neno hilo,alilitumia yeye mwenyewe akiwa
binadamu(Luka 7:48).
Luka
7:48
"Naye Yesu akamwambia yule mwanamke,umesamehewa dhambi zako"
"Naye Yesu akamwambia yule mwanamke,umesamehewa dhambi zako"
na
alitaka aendelee kulitumia hata utimilifu wa dahari katika hali ya
kibinadamu,ndio maana aliwaachia binadamu baada ya kifo chake ili waendeleze
kazi hiyo.
Kuondolea
watu dhambi ni moja ya utume wa Yesu(Marko 2:10),ni pamoja na kazi hiyo
aliwaachia mitume wake(Yohane 20:23).
Tukilinganisha
na mfano wa mtume Petro baada ya kumkana Bwana,tunaweza kujifunza kwamba
tunapoongea na Mungu peke yetu ni katika hali ya toba na majuto(Luka 22:61-62).
Luka
22:61-62
"Bwana akageuka na kumtazama Petro,naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana 'leo kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu' hapo akatoka nje,akalia sana."
"Bwana akageuka na kumtazama Petro,naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana 'leo kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu' hapo akatoka nje,akalia sana."
Hivyo
bado tunadaiwa kuungama iki kuondolewa dhambi zetu(Yohane 21:15-17)
Chakushangaza
ni kwamba,Wakristo wote tunaamini kwamba Sakramenti ya ubatizo inatuondolea
kabisa dhambi ya asili na dhambi zote zikizowahi kutendwa na yule anayebatizwa
na kwa kawaida huwa hatujibatizi wenyewe wala hatubatizwi moja kwa moja na
Mungu moja bali hubatizwa na wanadamu wenzetu.
Sasa
kama huyu mwanadamu mwenzetu anatubatiza na anatuondolea dhambi ya asili na
wote tunasadiki hivyo iweje tukija kwenye kitubio tunapinga ushiriki wa
binadamu mwenzetu na wakati matokeo yanayotarajiwa katika sakramenti hizo ni
yaleyale kama ya ubatizo.
Iweje
aliyekubatiza na kukuondolea dhambi ya asili na ukaamini kwamba amekuondolea
ashindwe au ushindwe kusadiki ushiriki wake katika kitubio?
Iweje
akisema "Nakubatiza kwa JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO
MTAKATIFU" hiyo iwe sahihi lakini akisema "Nakuondolea dhambi zako
KWA JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU" iwe sio sahihi?
Sasa
huoni kama unajipinga na kujichanganya mwenyewe hapo?
Wapendwa,tuache
kutafuta visingizio visivyo na ukweli kwaajili ya kutaka kupindisha ukweli.
Anayekuondolea
dhambi ni Mungu mwenyewe kupitia kwa wapakwa mafuta wake yaani mapadre ambao
amewaweka mwenyewe kwaajili ya huduma ya kanisa lake.
Wengine
hudai pia kwamba ni watu wote waliopewa jukumu hilo na sio mapadre pekee,lakini
ni vizuri kwanza kabla hujajitetea kwa msimamo huo dhaifu uchunguze tofauti
iliyopo kati ya "Wanafunzi" na "wafuasi" kisha usome Biblia
yako na kuona je jukumu hilo Yesu aliwatamkia wanafunzi wake au aliwatamkia
wafuasi wake.
Wanafunzi
wa Yesu ni wale kumi na wawili walioandamana naye.
Wafuasi
ni wale makutano wengi waliokuwa wakimfuata kwaajili ya kusikiliza mafundisho
yake.
Ikumbukwe
kwamba Yesu hakusema mambo yote hadharani mbele ya makutano,baadhi ya maagizo
msingi kama haya aliwachagua watu maalum kwaajili ya kuwapa kazi hizo na Biblia
inasema aliwaita faragha peke yao na kuwapa maagizo hayo.
Mungu
awabariki.
TUMSIFU
YESU KRISTO!
Nimeipenda, nikapenda na wewe uipate!!
Pd
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni