Baraza la Kipapa kwa ajili ya huduma za Kichungaji kwa Wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum, limetoa ujumbe wake kwa ajili ya maadhimisho ya Jumapili ya Utume wa Bahari ambayo ni Jumapili ijayo 10 Julai 2016. Ujumbe huo unatafakari umuhimu wa kazi za sekta ya bahari, katika mitazamo mbalimbali kama usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka sehemu moja hadi nyingine,ikiwemo usafiri wa watu, nguo, mafuta, magari na vyakula mbalimbali vilivyosindikwa na visivyo sindikwa , licha ya kazi za uvuvi zenye kutoa mazao mengi ya bahari ambayo ni sehemu muhimu ya matumizi katika chakula cha binadamu na wanyama wengine kila siku. Ujumbe unasema, bila uwepo wa bahari pia biashara ya kuagiza na kuuza nje ya bidhaa na mazao mengine isingekuwa rahisi.
Aidha umegeukia mtazamo wa ubinadamu katika maana ya matumizi ya vyombo vya usafiri vya majini, hasa katika umuhimu wake wa kuokoa maisha ya watu wengi walio katika hatari za kuangamia kama ambavyo inaonyesha kupitia kazi za kuokoa maisha ya maelfu ya watu wanaojaribu kuvuka bahari ya mediterranea wakiwa na tumaini la kuwa salama barani Ulaya, wakitumia hata vyombo hafifu visivyofaa na kupakizwa kwa msongamano mkubwa ndani ya vyombo visivyofaaa kuvusha watu.
Pia ujumbe unaendelea kutazama wingi wa watu wanaofanya kazi katika mazingira ya bahari wapatao atu karibia 1.200.000, kazi ya ubaharia na uvuvi , kutoka kila taifa (wengi wao kutoka nchi maskini) pia kukiwa na kundi la wafanyabiashara wasiopungua 50,000 ambao hutumia meli kusafirisha karibu 90% ya kila aina ya mizigo, na bila kusahau vikosi vinavyofanya kazi ya doria ya baharini, kwa ajili ya kufichua meli zinazotaka kufanya uhalifu bahari pamoja na mambo mengine yenye kuhatarisha usafiri na viumbe wa majini kwa njia moja au nyingine.
Na kwamba, daima maisha ya kimwili ya mabaharia yako hatarini kwa sababu mbali mbalimbali zinazotokana nguvu asilia za bahari, licha ya uharamia na wizi wa kutumia silaha.Pia maisha yao ya kuhama kutoka eneo moja hadi jingine daima huwahitaji kurekebisha mienendo yao kulingana na hali halisi za maisha mapya wanayokabiliana nayo, na hivyo huendelea kuwa tishio kubwa kwa usalama wa wafanyakazi wa baharini. Uwepo wao kisaikolojia daima ni hatarini katika maana kwamba, baada ya kuwa baharini kwa siku au wiki kadhaa wanapokataliwa mapumziko au meli kuzuiwa kuondoka, hupatwa na masononeko ya kunyimwa haki yao uhuru wa kupata huduma zote. .
Aidha ujumbe huu unatazama kwa kina maisha ya familia ya wafanyakazi wa meli ukisema, ni jambo la hatarini kutokana na mazingira ya kazi zao zinazo walazimisha kukaa mbali na familia zao na wapendwa kwa miezi mingi na wakati mwingine hata kwa kipindi cha miaka kadhaa, watoto wakikua bila uwepo wa ubaba na hivyo majukumu yote ya familia, huelemea katika mabega ya mama. Kutokana na hilo, heshima ya binadamu na utu wake katika kazi , huwekwa hatarini, hasa pale panapofanyika unyanyasaji wa kufanyishwa kazi kwa muda mrefu, ikiandamana na ucheleweshwaji wa malipo ya mishahara , na hivyo ikilazimisha wengine kuacha kazi bila kulipwa chochote. Baraza la Kipapa linaonyesha kujali tatizo hili na kusema, sheria za mabaharia ni lazima kuzingatia umuhimu wa kazi nyingi za baharia, kwa kuzitazama kwa kwa macho makali napia kujali uwepo wa shughuli zozote zisizo halali kuwa ni kosa la jinai hasa katika vitendo vinavyohusika na matukio kama vile meli kuzama , uchafuzi wa mazingira, n.k
Baraza la Kipapa likiwa limetiwa nguvu na Papa Francisko, aliyewaita Makasisi na watu wa kujitolea katika utume wa Bahari , kwamba wao ni sauti ya wote wanaofanya kazi mbali na wapendwa wao, na wale wote wanaoishi mbele ya uso wa hatari na hali ngumu, kwamba wao ni mitume wa Bahari wanaotakiwa kusimama imara upande wa mabaharia katika kusisitiza haki za binadamu na kazi zao katika ulingo wa Mabaria, kwamba ni lazima ziheshimiwe na kulindwa.
Na hivyo ujumbe umetoa wito kwa serikali zote na Mamlaka zote za bahari, kuimarisha utekelezaji wa Mkataba wa makubaliano ya ILO , wa mwaka 2006 kwa wafanyakazi wa bahari (MLC), hasa Kanuni ya 4.4 ambao lengo lake kuu ni kuhakikisha kuwa mabaharia wanaofanya kazi melini wanakuwa na haki za kupata mahitaji na huduma katika maeneo ya mwambao wanakotua, kwa ajili ya afya na ustawi wao.
Hatimaye, kwa ajili ya adhimisho la Jumapili ya Utume wa Bahari, ujumbe kwa mwaka huu, unalenga hasa kukumbusha jumuiya zote za Kikristo na kama mtu mmoja, umuhimu wa taaluma ya ubaharia na sekta ya usafiri wa meli katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo Baraza la Kipapa kwa ajili ya huduma za Kichungaji kwa wafanyakazi wa bahari, linatoa wito kwa maaskofu, hasa wale wa Jimbo la Utume wa Bahari, kuanzisha juhudi mpya za kipekee, kama ishara ya kuonekana ya upendo wao kwa wale ambao hawawezi kupata huduma za kawaida za Kichungaji kutokana na kazi zao za kushinda baharini.
Ujumbe umekamilka kwa kutoa shukurani za dhati kwa mabaharia wote kwa kazi zao na umewakabidhi mabaharia wote na familia zao chini ya ulinzi wa Mama Maria, Nyota ya bahari .
Ujumbe huu umetiwa saini na Kardinali Antonio Maria VegliĆ², Rais wa Baraza na Mons.Joseph Kalathiparambil Katibu wa Baraza hilo.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni