Tarehe Mosi Septemba, ambamo Mama Kanisa alifanya Maombi ya Kiekumeni kwa ajili ya Utunzaji wa Viumbe, Baba Mtakatifu Francisko alitoa ujumbe wenye kuhimiza kila binadamu atumie hekima na busara katika matumizi ya viumbe vya dunia yetu hii ambayo ni nyumba ya kawaida kwa viumbe wote. Siku hii ya dunia ya kuombea utunzaji wa viumbe , ilianzishwa mwaka 1989 na Patriaki Dimitrios I wa Kanisa la Kiotodosi la Costantinople
.
Katika mtazamo huo wa kujali utunzaji asili ya maumbile ya dunia, Baraza la Makanisa Dunia, WCC, kwa kushirikiana na Mtandao wa Maombi wa Papa Francisco na vikundi Katoliki vinavyosjishughulisha na hali ya hewa, duniani, kwa pamoja wameunda ukurasa wao katika mtandao ambamo wametoa mwaliko kwa Wakristo wote kushiriki katika utunzaji wa viumbe kwa njia mbalimbali , ikiwemo utoaji wa taarifa za mipango ya sala za kuombea utuzaji wa viumbe na kutoa habari mbalimbali kufanikisha uhamasisha kampeni ya wiki moja , kwa ajili ya kuleta mwako zaidi katika kutunza viumbe.
Papa Francisco katika ujumbe wake, anatoa mwaliko kwa watu wote kusikiliza kilio cha aridhi kinachotokana naaridhi kuchakazwa na matumizi mabaya ya binadamu, na pia kusikiliza kilio cha watu maskini wanaoishi katika hali za kugandamizwa na mabwanyenye wanaotumia vibaya rasilimali. Papa amessisitiza mabadiliko katika utendaji wa binadamu katika masuala yanayohusu aridhi na mazingira.
Amesema tukiwa tumeungana pamoja na waamini wenzetu wa Makanisa ya Kiotodosi , na makanisa mengine ya Kikristo , katika siku hii ya kuombea utunzaji wa maumbile duniani, kila muumini na watu wote kwa ujumla, tunaalikwa kutoa ahadi kwa mara nyingine , kuwa mawakili wa viumbe, kumshukuru Mungu kwa kazi ya ajabu ya mikono yake , alizozikabidhi chini ya huduma ya binadamu. Na hivyo tunahimizwa kuomba msaada wake kwa ajili ya kuvitunza na kuvilinda viumbe, na pia kuomba msamaha kwa dhambi tulizofanya dhidi ya dunia yetu hii tunamoishi.
Baba Mtakatifu Frnvcisko ametoa shukurani zake kwa juhudi hizi za Kanisa na jamii za Kikristo, kwa kuungana pamoja na dini nyingine ,kukumbushana yanayopaswa kufanyika ili dunia iendelee kuwa makazi ya viumbe katika asili yake. Ameitaja siku hii kuwa ni siku ya kukumbushana tunavyopaswa kuheshimu mazingira na kujiepusha na hatari ya unyonyaji na ukosefu wa uwajibikaji katika kuitunza dunia yetu, kama alivyoonya mwanzilishi wa juhudi hizi , Patriaki Dimitrios I wa Constanople miongo kadhaa iliyopita.
Papa amesema, inatia moyo kwamba , dunia nzima, inaonyesha kujali juhudi hizi zinazolenga kukuza haki za mazingira, kuhofia hali ya maskini na kuwajibika na ahadi ya jamii katiak kutunza mazingira na kutoa wito wa kukusanyika pamoja na hasa vijana, wa tamaduni mbalimbali za kidini. Papa anatumaini kwamba , siku hii itaweza kuwa kichocheo cha kuhimiza utendaji wenye kujali na kuihurumia dunia kama makao yetu ya kawaida ya wote, ambamo tunapaswa kukumbatia misingi ya kuishi kwa umoja na mshikamano wa kugawa kile kinachopatikana kama washarika.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni