Ijumaa 02.09.2016, Wadomenikani walifungua Kongamano lao la VII, kama sehemu ya mwendelezo wa Mradi wao wa Salamanca , wenye kujumuisha viongozi wa ngazi za juu wa shirika kwa ajili ya kutafakari azma yao ya kutetea haki za binadamu, wakitazama wakati uliopita, wakati wa sasa na wakati ujao.
Kongamano hili linaendelea hadi siku ya Jumatatu 05.09.16 linafanyika katika mji wa Salamanca Hispania, na linahudhuriwa na Wajumbe Wadomenican zaidi ya 200 kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Na kwamba sehemu iliyochaguliwa kufanyika Kongamano hili ,ni nyumba ya Watawa ya Mtakatifu Stephano , iliyotumiwa na Watawa karne ya 14 kwa ajili ya utetezi wa haki za watu mahalia wa Amerika ya Kusini. Kongamano linaendelea kuzungumzia hadi leo uhusiano kati ya elimu na umisionari kwa Wadomenikani, wakiainisha hasa maisha ya kitume na elimu
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni