0
Alama za kuonesha mwendo tempo. Za msingi bi allegro, largo, adagio, vivace, presto, andante na lento. Alama hizi zinafuata idadi ya noti katika dakika (bpm - beats per minuet au MM - metronome)
Tuanze na alama yenye kasi sana na kushuka mpaka mwendo pole.
1. Prestissimo yaani haraka sana. Hii humaanisha iwapo time signature inaonesha 2 4 basi ina maana imba crothets 200 - 208 ndani ya dakika moja. Wafananao na mwendo huu ni vivacissimo na allegrissimo.

Alama ifuatayo kwa kasi ni presto - haraka. Hii huimbwa mf katika 2 8 ina maana ni quavers 168 - 200 ndani ya dakika moja. Afananaye ni vivo.
3. Vivace - kwa kuchangamka imba aina ya noti tajwa 140 kwa dakika.
4. Allegro- haraka, imba noti tajwa 120 - 168 kwa dakika. Chini yake ni allegretto.
5. Moderato - mwendo wa kadiri, imba noti tajwa 108 - 120 ndani ya dakika.
Chini yake ni andantino
6. Andante- mwendo wa kutembea, imba noti tajwa 76 - 108 ndani ya dakika moja.
Chini yake ni adagietto.
7. Adagio - mwendo pole, imba noti tajwa 66 - 76 ndani ya dakika moja.
8. Larghetto - mwendo pole zaidi, imba noti tajwa 60 - 66 ndani ya dakika moja.
Chini yake ni Lento - mwendo pole mzito.
9. Largo - mwendo pole mzito, imba noti tajwa 40 - 60 kwa dakika.
Chini zaidi ni
Lentissimo
Adagissimo
Largissimo
Range inayowekwa ni kwa ajili ya kuitikia alama mbalimbali za wakati. Wastani ukiwa ni mwendo unaohusisha robo noti (crotchet)
Kumbuka suffix -issimo na etto (mwishoni) aidha unaongeza (amplify) ama kupunguza (diminish) upole na uharaka wa mwendo husika.
UBADIKIKAJI WA MWENDO katika mwendo uliotajwa hutumia terms zifuatazo:-
Accelerando (accel)- ongeza mwendo tokea noti iliyowekewa neno hilo (speed up)
Ritardando (fit. au "ritard." - nukta kwenye ritard(.) iiumbukwe. - punguza mwendo (delaying)
Meno Mosso - punguza uharaka, nenda taratibu. (Kumbuka maneno yote kuanza na herufi kubwa. Sio Meno mosso bali Meno Mosso)
Piu Mosso - ongeza uharaka, wepesi wa mwendo - kimbia.
Rallentando - punguza mwendo hasa mwishoni mwa section ya wimbo (rall.)
Ritenuto (riten.) - punguza mwendo kidogo (sio kidogo kidogo - poco riten.) bali punguza usiwe kadiri ulivyokwenda mwanzi kabla ya alama.
Kumbuka Ritenuto sio Ritardando. Hii hufupishwa - rit.
Stretto - kimbia kidogo kwa muda ( rushing ahead)
Rubato - ibia (iba) muda kwa muda kama unafanya adjustment kwa ajili ya kuelezea (mkazo / sisitiza) jambo.
Ukiwa na alama mbili na unataka kurudi kwenye mwendo wa mwanzo utatumia neno 'A tempo' yaani rudi kwenye base tempo (mwendo msingi).
Iwapo unebadilibadilisha mwendo sana katika ya wimbi na unataka kurudi kwenye base tempo tumia "Tempo Primo" ama 
"Tempo I". Mfano wimbo ulianza Moderato baadaye ukaingia Allegro baadaye Lento hivyo utaandika "Tempo Primo" yaana "mwendo wa awali"

Na. Beatus Idama


Chapisha Maoni

 
Top