1. Nyimbo zifuate vipindi vya mwaka wa liturujia wa Kanisa na ziwe sahihi kufuata misale ya altare na kitabu cha masombo pamoja na kalenda ya liturujia.
2. Zichaguliwe nyimbo zinazoweza kuimbwa kwa urahisi na zinazowashirikisha waamini wanaoshiriki adhimisho
3. Nyimbo zichukuliwe kutoka vitabu vilivyokubaliwa na Kanisa(vilivyo haririwa na kupata ithibati)
4. Nyimbo mpya hasa zile zilizotungwa na watunzi wasiosoma teolojia zihaririwe na kamati ya Liturujia na Muziki Mtakatifu tena ziwe chache katika adhimisho moja.
5. Nyimbo ziimbwe mara nyingi ili ziweze kuimbwa na waamini wote.
6. Nyimbo zipangwe kulingana na matukio yalivyo katika Misa. Yaani kila kipengele ziimbwe nyimbo zinazoeleza tukio linalofanyika wakati huo katika Misa ili kupatanisha maneno yanayo imbwa na tendo linalofanyika.(Sadaka, Komunyo, Shukrani). Ni vema kuwa makini hasa nyakati za sherehe – Pasaka, Noeli, Ndoa, Upadre nk. Mfano; haileti mantiki wakati wa komunyo kuimba (KISURA WANGU NAKUPENDA hata kama siku hiyo ni ndoa).
7. Kwaya ya kanisa ijaribu kuepuka kabisa melodia na maneno yasisiyo fadhili utamaduni wa kanisa katoliki.
8. Ala za muziki: Ala rasimi katika kanisa ni kinanda. Ala nyingine kama vile ngoma zakupigwa kwa mkono, kayamba, na marimba nk zisiachwe kwani zinadumisha utamaduni wetu.
9. Wapiga vipiga ala: Wafanye maandalizi vizuri, wapige ala kwa busara, kiufundi, na kwa kiasi ambacho sauti zake hazigeuki kuwa “makelele”
10. MAVAZI YA WANAKWAYA. Sare za kwaya zisishonwe kwa mtindo unaofanana na nguo za Kikuhani zitumikazo wakati wa Misa au nguo za Watawa. Mtindo mwingine unaweza kutumika. Zishonwe katika mtindo ulio rahisi kwa rangi mbalimbali za kiliturujia.
11. Dansi/ Kucheza. Mapokeo ya Kanisa yanatuongoza kuwa katika Liturujia tunahitaji utulivu wa aina ya pekee. Kucheza kuwe kwa kiasi tena kwa maeneo machache. Waimbaji ni sehemu ya kanisa linalo Sali. Sare na umoja wa matendo, maneno na mkao vinahimizwa. Waimbaji wawaongoze waamini kufuata utaratibu wa Misa(kusimama,kukaa, kupiga magoti nk)
Na Fr. Mwageni Deo
(Kny. Kamati ya Muziki Mtakatifu)
(Kny. Kamati ya Muziki Mtakatifu)
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni