0
KRISTO!
Hii ni list ya mambo machache ambayo yakifanyiwa kazi yatatengeneza kwaya bora sana:

1. Wanakwaya *wote* wanaheshimu mazoezi kwa kuhudhuria, tena kwa wakati, na bila visingizio?
2. Endapo wanakwaya wengi wanashindwa kufika mazoezini kwa wakati, uongozi unaangalia namna ya kuhakikisha kwamba tatizo hilo linarekebishwa ili kuwawezesha wawepo mazoezini kwa wakati?
3. Kila mwanakwaya anabeba jukumu la kujifunza kwa bidii yeye mwenyewe kwanza badala ya kungojea "nguvu ya umma"?
4. Mwalimu anahakikisha kwamba kila mwanakwaya anajengwa kiuimbaji badala ya kukaririshwa nyimbo?
5. Uongozi wa kwaya na Kamati ya ufundi ya kwaya hukaa pamoja na kupanga mipango ya maendeleo ya kiuimbaji kabla ya mwaka kuanza, na kukaa kutathmini utekelezaji kila mwisho wa mwaka?
6. Kwaya inawasiliana mara kwa mara na Paroko ili kupata mwongozo wa kiliturjia katika uimbaji?
7. Kwaya ina utaratibu wa kuomba Semina/Mafungo ili kuhakikisha kwamba wanakwaya wanakomaa kiroho?
8. Kwaya ina mipango madhubuti ya kujitengenezea kipato ili iweze kukidhi mahitaji yake ya kiuendeshaji badala ya kuombaomba kila kitu kwa wafadhili?
9. Kwaya ina kawaida ya kufanya mazoezi ya waimbaji na wapiga ala kabla ya siku ya Ibada?
10. Wapiga ala wanapata muda wa kutosha kujifunza na kufanya mazoezi?
Kama majibu ya maswali yote ni *ndiyo*, basi kwaya yako iko pazuri sana, ila usibweteke; kaza buti zaidi!
Endapo kuna majibu kadhaa au mengi, au yote ya *hapana*, usikate tamaa; anza kufanyia kazi moja hadi jingine; penye nia na unyofu wa moyo, Mungu huonesha njia!
By...DEo Mhumbira

Chapisha Maoni

 
Top