0
Jumatatu 26 Desemba wakati Kanisa linasherehekea sikukuu ya Mtakatifu Setefano, Baba Mt Francisko katika sala ya Malaika Bwana alitoa mahubiri kwa mahujaji wote waliofika viwanja vya Mtakatifu Petro akisema:
Furaha ya kuzaliwa kwa Bwana inatujaza mioyo yetu hata leo, wakati liturjia ya siku inaadhimisha mfiadini Mtakatifu Stefano, shahidi wa kwanza  mkristo, na kutualika , tuige mfano aliyotuachia wa  kujitoa sadaka .

Ni ushuhuda mtakatifu hasa wa kishahidi kwa  Kristo, aliyeteseka kwa upendo wa Yesu Kristo, na  ni kifodini kinachoendelea kuwepo katika historia ya Kanisa kuanzia kwa Stefano hadi  nyakati sasa.Ushuhuda huo umetokana katika maelezo ya Injili ya ( Mt 10,17-22). Yesu anapowatangazia mitume wake yale atakayokumbana   wakati wa utume wake  yaani, kukukataliwa na watu na kuhukumiwa kifo,  na aliwapa  tahadhari yakuwa "nanyi  mtachukiwa na kila mmoja kwa jina langu" (Mt 10,22).
Papa aliendelea kusema; ulimwengu unawachukia wakristo  kwa  sababu zilezile  walizo mchukia Kristo kwani Yeye alileta mwanga wa Mungu na ulimwegu ukapendelea giza  ili kuendelea kuficha mambo yao mabaya. Kwa namna hiyo kuna malumbano kati ya mafundisho ya Injili na fikra za kiulimwengu. Kumfuata Yesu maana yake ni kufuata mwanga , uliyo angaza usiku huko Betlehemu  na kufukuza  kwa  mbali giza la ulimwengu.
Mtakatifu  Stefano akiwa amejazwa na Roho Mtakatifu , alishambuliwa wa kupigwa mawe kwa sababu ya imani yake kwa Kristo mwana wa Mungu  na Mzao wa kwanza aliyekuja duniani , ambaye  anamkaribisha kila mmoja  kuchagua mwanga na maisha.Na ndiyo sababu moja msingi iliyo mfanya Yeye aje kwetu.
Kwa maana hiyo Mtakatifu Stefano akiwa  anampenda Bwana na  kusikiliza sauti yake, alichagua Kristo, ambaye ni maisha na mwanga kwa kila binadamu. Kitendo cha kuchagua ukweli, yeye aligeuzwa wakati huo huo sadaka yenye  fumbo la ubaya linaliendelea hata leo hii katika ulimwengu huu.
Baba Mtakatifu alibainisha ubaya huo akisema  ; Hata leo  hii kutoa ushuhuda wa mwanga na ukweli,Kanisa linafanya uzoefu katika sehemu tofauti ulimwenguni, ya kuchukiwa, misukosuko  hadi kufikia majaribu ya kifodini. Alisema ni ndugu wangapi  na kaka wanaendelea kubaguliwa  na kuteswa   kwaajili ya Kristo: Na kuongeza “Leo hii tuwafikirie ikiwa ni njia ya kuwa pamoja nao karibu kwa upendo kwa njia ya sala zetu na machozi yetu vilevile hatuna budi kutoa nafasi ndani ya mioyo yetu kwaajili ya Mwana wa Mungu anayejitoa sadaka katika sikukuu ya Noel, tuifanye upya furaha na utashi wa kutafuta Yeye awe  kiongozi pekee katika maisha yetu , kwa kusali na kuishi kwa fikra za kiinjili ,tukitupilia mbali fikra za utawala wa ulimwengu huu.
Kwa maombezi ya Bikiara Maria Mama wa Mungu na wa mashahidi , tuinue sala zetu , ili aweze kutuongoza na kutusaidia daima katika safari yetu ya kumfuasa Yesu Kristo tunaye muabudi katika pango na ambaye ni shuhuda mwaminifu wa Mungu Baba.
SALA BAADA SALA YA MALAIKA WA BWANA
Baada ya Angelus Baba Mtakatifu aliwasalimia mahujaji wote akisema “ katika furaha hii ya kuzaliwa kwa Bwana ninawasalimieni nyote mliofika kutoka Italia na sehemu mbalimbali za ulimwengu, na kuwatakia tena amani na utulivu, viwatangulie katika familia zenu kwenye siku hizi za furaha na za kindugu, na kwa namna ya pekee heri ya wote mnaoitwa kwa jina la Stefano na Stefania!”

Aidha alisema, “ katika  siku hizi nimepokea  ujumbe wa heri nyingi za sikukuu kutoka ulimwenguni kote na kutokana na ukosefu wa muda wa kuwajibu wote , ninawashukuru wote  na hasa zawadi ya sala zenu mnazoniombea. Alimalizia “ kwa moyo wote  Mungu awaongeze kila jema kwa wema wenu.”
Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican


Chapisha Maoni

 
Top