0
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Nchi ya Congo (DRC) Askofu Mkuu Marcel Utembi Tapa alitoa wito kwa vyama vya upinzini kufanya mazungmzo na makubaliano  kwaajili ya usimamizi wa kipindi cha mpito  ,hayo  ni kwasababu ya kutaka suluhisho la   mgogoro wa kisiasa nchini humo kutokana na Rais wa nchi hiyo  kumaliza muda wake

.
Aliyasema hayo wakati wa kumalizia kikao cha Baraza la Kitaifa la Viongozi wa Kidini la Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo CENCO, linalosimamia upatanishi kati ya serikali na upinzani, na kutoa pendekezo la kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo Alhamis 21 Desemba 2016.
Nia ya  Maaskofu wa Kanisa la Katoliki, wanatafuta namna ya kuweza kutatua mizozo iliyopo ndani ya nchi, kwani hadi hivi sasa tofauti kuu iliyopo ni juu ya mamlaka ya Rais Joseph Kabila wakati wa kipindi cha mpito, baada ya muda wake rasmi  kumalizika 19 Desemba mwaka huu.
Vyama vikuu vya upinzani vilivyoungana chini ya jina jipya la Rasemblement walisusia mazungumzo yaliyoongozwa na Umoja wa Afrika,na kutaka serikali ya mpito ikiwa itaongozwa na Kabila au la ni lazima ipunguze sana madaraka ya kiongozi huyo.
Halikadhalika upinzani unataka uchaguzi ufanyike mnamo mwaka ujao wa 2017, huku serikali na baadhi ya vyama vya upinzani vinataka uchaguzi ufanyike 2018.Na Habari kutoka UN sinasema baada ya miaka 10 ya kuongoza Umoja wa Mataifa, Kiongozi Ban Ki –Moon atahitimisha jukumu hilo tarehe 31 Desemba 2016.
Akizungumza kwenye mahojiano yake ya mwisho na Idara ya Habari ya Umoja wa Mataifa, Ban alisema ilikuwa ni heshima kubwa kwake yeye kuongoza taasisi hiyo katika muongo mmoja uliokabiliwa na changamoto kali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi na mizozo .
"Kwa mtazamo wangu kama Katibu Mkuu wakati wa uongozi wangu nikishughulikia mizozo hapa na pale, nimeona kuwa migogoro haisababishwi na wananchi. Migogoro mingi kwa bahati mbaya inasababishwa na viongozi, kwa sababu viongozi wengi hawaonyeshi nia ya dhati kuzingatia malengo na misingi ya katiba ya Umoja wa Mataifa na haki za binadamu. Ndio maana wananchi wanakuwa na hasira na wanapinga uongozi wao."
Aidha na kusema, ndio maana amekuwa anasihi viongozi kuweka mbele maslahi ya umma akiwaeleza kuwa iwapo wangalikuwa na mshikamano na raia wao, mizozo ingalikuwa michache hivi sasa.
Halikadhalika alielezea baada ya kuhitimisha jukumu lake kitakachofuatia ni,  "Mimi ni mtu ambaye niko tayari kwa mawazo mapya. Kama Katibu Mkuu mstaafu bila shaka nimejifunza mambo mengi na maono na ufahamu. Chochote kitakachokuwa cha lazima, popote pale itakapokuwa lazima, sitasita kufanya jambo jema kwa nchi yangu au hata jamii ya kimataifa zaidi ya nchi yangu Korea. Nadhani hilo ni jambo jema kwa katibu mkuu mstaafu kupeleka usaidizi wake kwa jambo jema."
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

Chapisha Maoni

 
Top