0
Tarehe 21 Desemba 2016 Baba Mtakatifu Francisko  alikutana na Kardinali Angelo Amato Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwaajili ya kuwatangaza wenye Heri na watakatifu.Katika mkutano wao ametoa ruhusa ya kuwatambua na kuwatangaza watakatifu,na wenye heri  wafuatao:  

—  Mwenyeheri Faustino Miguez, Padre na Mtawa  wa Shirika la Masikini wa Mama wa Mungu kwa jina jingine  (Scolopi),na mwanzilishi wa Shirika la watawa wa kike (Calasanziane ) wa watoto wa Mungu mtume; alizaliwa 24 machi  1831 na kifo chake 8 machi  1925; 
—   Mtumishi wa Mungu  Leopoldina Naudet, Mwanzilishi wa Shirika la watawa wa kike wa Familia Takatifu ; alizaliwa  31 mei  1773 kifo chake 17 agosti 1834.

— Mashahidi wa watumishi  Mungu Matteo Casals, Padri na mtawa , Teofili Casajús, mwanafunzi wa nadhiri, Ferdinando Saperas, ndugu aliyefunga nadhiri , na wenzao  106 wa Shirika la Wamisionari wa watoto wa Moyo safi wa Bikira Maria;   waliuwawa kwa  chuki  ya kutetea imani yao wakati wa vita ka ya mwaka  1936 na  1937;huko Hispania.
—Mtumishi wa Mungu Giovanni Battista Fouque, Padri wa Jimbo ;aliyezaliwa  il 12 septemba  1851 na kifo chake  5 desemba  1926.
— Mtumishi wa Mungu  Laurent  wa Roho Mtakatifu  (enzi  zile : Egidio Marcelli),  mtawa  wa  Shirika la la Mateso ya Yesu Kristo ; aliyezaliwa 30 agosti 1874 na kifo chake  14 oktoba 1953;
— Mtumishiwa Mungu  Maria Raffaella wa Moyo Mtakatifu wa Yesu   (wakati ule : Sebastiana Lladó y Sala), Mwanzilishi wa Shirika la Wanisionari wa Mioyo ya Yesuna Maria;  aliyezaliwa  2 Januari 1814 na kifo chake 8 machi 1899;

— Mtumishi wa Mungu  Clelia Merloni, Mwanzilishi wa  Shirika la mitume wa Moyo Mtakatifu wa Yesu ; aliyezaliwa 10 machi 1861 kifo chake 21 novemba 1930;
— Mtumishi wa Mungu  Isidoro Zorzano Ledesma, mlei , wa Shirika la Msalaba Mtakatifu na Opus Dei; aliyezaliwa  13 septemba  1902 na kifo chake  15 Julai 1943.
 Sr Angella Rwezaula  Idhaa  ya Kiswahili ya Radio Vatican.

Chapisha Maoni

 
Top