Kardinali Agostino Vallini, Makamu Askofu Jimbo kuu la Roma amewaandikia Wakleri wote wa Jimbo kuu la Roma kushiriki na Baba Mtakatifu Francisko katika kipindi cha sala, tafakari na adhimisho la huruma ya Mungu inayomwilishwa kwa namna ya pekee kabisa katika Sakramenti ya Upatanisho, Alhamisi, tarehe 2 Machi 2017 Saa 3:30 za asubuhi kwa saa za Ulaya, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu
Askofu msaidizi Angelo De Donatis aliyepewa dhamana ya kuratibu na kusimamia majiundo endelevu ya Wakleri, ataongoza Ibada ya Toba na baadaye kufuatiwa kwa kipindi cha maungamo. Ni matumaini ya Kardinali Vallini kwamba, Wakleri wengi wataweza kuhudhuria tukio hili kama kielelezo cha umoja na sala kumzunguka Baba Mtakatifu Francisko ambaye pia ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Roma!
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni