
Wengine watatangazwa watakatifu tarehe 15 Oktoba 2017 ambao ni Angelo da Acri Padri wa Shirika la ndugu wadogo Wakapuchini aliyezaliwa Oktoba 1669 na kifo chake 30 Oktoba 1739. Faustino Míguez, padre wa Shirika la Scolopi na mwanzilishi wa Shirika la Calasanziano wa watawa wa kike Mchungaji mwema;
Mwenye heri Andrea de Soveral na Ambrogio Francesco Ferro,mapadre wa Jimbo na Matteo Moreira, mlei na wanzake 27 mashahidi waliouwawa kwa ajili ya kutetea imani yao nchini Brazil tarehe 16 Julai 1645 na tarehe 3 Oktoba 1645. Na mwisho Cristoforo, Antonio na Giovanni, vijana mashahidi walio uwawa kwa ajili ya kutetea imani yao nchini Mexco mwaka 1529.
.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni