Ni ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa Kenya uliotolewa na Fides hivi karibuni ambapo Maaskofu wa Kenya wanaelezea wasiwasi wao kuhusu mvutano wa kisiasa unao athiri nchi yao. Maaskofu hao wanaeleza kuwa uchaguzi wa hawali uliofanywa na chama kimoja kimoja kuchagua wagombea wa kuwasilisha katika uchaguzi Mkuu mwezi Agosti,umekuwa na sifa ya udanganyifu, mvutano na vurugu.
Bara la Afrika linakabiliana na mgogoro mbaya zaidi wa chakula kwa mihongo pia dharura kutokana na ukame. Maaskofu wanashutumu vingozi wakisema, hilo ni janga lakini ni pamoja na viongozi wenyewe kwasababu wanapoteza rasilimali chache zilizopo kununua kura. Kwa njia hyo katika ujumbe wanasema, utamaduni wa uchoyo na ubaguzi unazidisha hali ya sasa kuwa ngumu na ndiyo maana wakenya sasa wana msukumo wa nguvu wa mawazo ya kukata tamaa.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni