0

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 4 Mei 2017 amekutana na kuzungumza na  Bi Aung San Suu Kyi, Mshauri wa Nchi na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Watu wa Myanmar na ujumbe wake! Taarifa iliyotolewa na Vatican inaonesha kwamba, Jamhuri ya Muungano wa Watu wa Myanmar pamoja na Vatican wamekubaliana kimsingi kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili. Vatican itafungua ubalozi wake nchini Myanmar na Myanmar kwa upande wake itafungua ubalozi wake mjini Vatican

Chapisha Maoni

 
Top