0
WAAMINI  wakatoliki   wa  Chama cha kitume cha Karismatiki wameshauriwa kuacha kuweka masharti  kwa  wahitaji wenye shida mbalimbali  ambao wanawafanyia maombi ya  uponyaji    sanjari na malipo ya aina yeyote na badala yake  waendelee kutoa huduma kwa ujenzi  wa Kanisa kadiri ya sheria, kanuni na taratibu za Kanisa Katoliki. 
Wito huo umetolewa na Padri John Maxwell Quiye kutoka nchini  Ghana  wakati wa Kongamano kubwa la chama hicho Jimbo Katoliki Mbeya na majimbo jirani ya Iringa na Njombe lililofanyika  katika viwanja vya Ruanda Nzovwe, jimboni Mbeya  na kuhitimishwa Jumapili  iliyopita.

Chapisha Maoni

 
Top