Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo amemkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, kisima cha maji katika
kituo cha mafunzo cha watoto (Mahabusu ya watoto) Upanga jijini Dar es salaam.
Kardinali Pengo amekabidhi mradi huo uliotokana na michango iliyotolewa na
Watoto wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu Jimbo Kuu Katoliki Dar es
salaam, ambapo hadi kukamilika kwake mradi huo umetumia jumla ya shilingi
Milioni 11,780, 000/=. (Na Pascal Mwanache
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni