TAARIFA YA MARIATHON 2017
JUNE 16, 2017
Mpendwa mdau na msikilizaji wa Radio Maria, Sauti ya Kikristu Nyumbani Mwako,
Tumsifu Yesu Kristu!
Ninayo furaha kubwa kuwa tena pamoja nawe leo, kwa lengo la kuhitimisha kampeni yetu ya Mbio za Mama kwa mwaka huu zijulikanazo kwa jina la Mariathon 2017, zilizo zinduliwa rasmi April 28 na kuhitimishwa Juni 12, 2017.Mpendwa Msikilizaji wangu, Napenda kuchukua fursa hii ya pekee kukushukuru sana, Kwa mapendo yako kwa Radio ya Mama yanayoandamana na majitoleo yako, daima tumekuwa tukiuona wema wa Mungu ukitenda kazi katika chombo hiki cha Mama yetu Bikira Maria.
Nichukue fursa hii kuwashukuru wadau wetu wote waliojitoa kwa hali na mali kuhakikisha Mbio hizi zinaendelea kwa mafanikio makubwa. Nawashukuru sana Mababa Maaskofu wote, Mapadre, watawa wote wa kike na wa kiume, Viongozi wa Marafiki wa Radio Maria ngazi za Jimbo, Parokia na Klabu zote, wadau wetu wote na watumishi wote wa Mama hapa makao makuu na kwenye mikoa yote kwa jinsi mlivyoweze kushiriki kwa unyenyekevu na kujitoa bila kujibakiza ili kufanikisha kampeni yetu hii, sina la ziada la kuwaambia zaidi ya kusema kwa unyenyekevu kabisa, Asanteni sana, na tunazidi kumuomba Mungu ili kila ulichokipunguza kwa ajili ya kufanikisha kampeni hii, akurudishie kadiri ya haja ya Moyo wako.
Msikilizaji wangu Mpendwa, kabla ya kupitia matokeo ya mbio zetu, ni vyema tukajikumbusha malengo yetu tuliyo yaleta kwako siku ile ya Uzinduzi tarehe 28 April 2017.
Mpendwa msikilizaji wangu, mwaka huu tulikuja kwako na kukuomba uiwezeshe Radio yako kiasi cha Shilingi za Kitanzania milioni 450 ambazo ni kwa ajili ya nia zifuatazo; Shilingi milioni 50 kwa ajili ya kulipia ada za masafa ya Radio kwa Tanzania bara na Visiwani, Shilingi milioni 160 kwa ajili ya manunuzi na maboresho ya mitambo yetu, Shilingi milioni 150 kwa ajili ya ada ya Umisionari, na Shilingi milioni 90 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Radio kwa mwezi Mei 2017.
Katika kampeni hii tulitumia njia mbali mbali kukusanya michango toka kwa wadau wa Utume wa Radio Maria. Njia hizo ni pamoja na Ziara mbali mbali maparokiani, kwenye jumuiya ndogondogo na pia kwenye familia mbali mbali huku tukisali na kumshukuru Mungu kwa pamoja. Tulitumia pia njia ya simu za mikononi, yaani ile akaunti yetu ya 100200, Bahasha, benki na Uchangiaji kwa njia ya mtandao yaani “Online Donation”.
Baada ya utangulizi huo, naamini lazima utajiuliza swali lifuatalo, Je, tumeweza kweli kukusanya fedha za kutosha kugharamia malengo yetu hayo? Kwa majibu sahihi karibu sasa tuipitie taarifa yetu kwa pamoja.
Naomba pia niwakumbushe kwamba, wakati tunaanza mbio zetu tuligawana malengo kimikoa kwa kufuata vigezo mbalimbali. Lengo likiwa ni kuhakikisha kila mkoa unashiriki mbio hizi kulingana na hali halisi ili iwe rahisi kupima uwezo wa kukimbia kiushindani. Karibu usikilize msimamo wa mbio zetu kwa kufuata kigezo cha mwendo kasi katika kumaliza lengo la mkoa na au Jimbo;
Asante Sana kwa kujitoa kwako na kutenga muda wako adimu kuisikiliza taarifa yetu ya leo. Kama wasemavyo wahenga, kushukuru ni kuomba tena, basi nikuombe tena tuendelee kuipenda, kuisikiliza na daima kuiwezesha Radio Maria ili kwa kupitia chombo hichi, tuweze kutimiza majukumu yetu ya uinjilishaji na zaidi sana kuupata utakatifu tunao utamani.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni