0


Ninawakaribisheni nyote na kumshukuru Rais  wa Kituo cha Liturujia Askofu Caludio Maniago kwa hotuba yake na maneno aliyotoa kuwasilisha Wiki hii ya Liturujia Kitaifa nchini Italia ikiwa pia  ni miaka 70 tangu kuanzishwa kwa kituo cha utendaji wa Liturujia. Ni maneno ya utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 24 Agosti  2017 alipokutana na wajumbe wa Mkutano wa Wiki ya Liturujia wakiwa katika siku yao ya mwisho ya kufunga wiki ya Mkutano huo. Hiki ni kipindi ambacho katika historia ya Kanisa kwa namna ya pekee katika historia ya Liturujia yametokea matukio mengi msingi na siyo ya kijuu juu. Siyo rahisi kutokukumbuka Mkutano Mkuu wa Mtaguso wa II wa Vatican, kama vile pia katika  kukumbuka mageuzi ya kiliturujia yaliyopita.
Baba Mtakatifu anasema; haya ni matukio mawili yanayo ungana moja kwa moja, Mtaguso Mkuu na mageuzi ambayo haya kujitotokeza mara moja, bali yamepitia katika hatua mbalimbali za maandalizi ya muda mrefu. Hiyo inashuhudiwa na kile kiitwacho harakati za kiliturujia na majibu yaliyotolewa na mababa watakatifu kutokana na utambuzi wa usumbufu katika sala za Kanisa. Hiyo ni kwasababu Baba Mtakatifu Francisko anafafanua; unapotambua haja ya kitu fulani hata kama ufumbuzi siyo wa haraka, lakini hipo haja ya kujiweka katika mwendo ili kutafuta ufumbuzi unaotakiwa.
Baba Mtakatifu anafikiria Mtakatifu  Pius X  aliyepanga kwa upya miziki mitakatifu na kurejesha maadhimisho ya Jumapili, wakati huo huo  aliunda tume ya mageuzi ya Liturujia kwa ujumla akitambua nini kingetokea, hasa zaidi kazi kubwa na  muhimu  iliyokuwa lazima itekelezwe. Kwa njia hiyo yeye mwenyewe alitambua hata ulazima wa kupita miaka mingi kabla ya muundo kamili wa Liturujia kufanyika na ambayo ilionekana tena kuwa mpya yenye kung’aa katika hadhi yake na utulivu mara baada ya kuwa imesafishwa ule uzee wake.
Baba Mtakatifu anazidi kufafanua; Mpango wa Mageuzi aliouchukua Pius XXII, kwa Waraka wa Mungu mpatanishi “Mediator Dei” na kuanzishwa kwa tume ya mafunzo ya utafiti;hata hiyo ilichukuliwa maamuzi madhubuti kuhusu toleo la kitabu cha masifu ya sala (Zaburi), kuweka kufunga na matumizi ya kugha hai katika maadhimisho, umuhimu wa mageuzi ya mkesha wa Pasaka na Wiki Takatifu. Kutokana na msukumo huo kufuata mfano wa nchi nyingine, ndipo kulitokea katika nchi ya Italia Kituo cha Kiliturujia kikiongozwa na Maakofu kuwakumbusha watu waliokabidhiwa kwao na kuongozwa na mafunzo ya Kanisa pamoja na uchungaji wa kiliturujia. Leo hii bado kuna haja ya kufanya kazi katika mweleko hasa kuweza kugundua misingi ya maamuzi yaliyotolewa wakati ule na mageuzi ya kiliturujia, haja kushinda namna ya mitazamo ya kijuu juu tu au mapokezi na mazoea yanayo haribu sura ya liturujia. Hii haina maana ya kufikiria upya mageuzi kwa kupitia upya maamuzi, bali ni kutambua vema sababu msingi zilizowekwa ikiwa ni pamoja na kupitiatakwimu na rekodi za kihistoria, aidha kujikita kwa kina zile kanuni na kuchunguza nidhamu inayotawala.
Baba Mtakatifu Francisko pamoja na hayo yote anasema, lakini kwasasa, baada ya mafundisho ya mwendo mrefu tunaweza kusema kwamba mageuzi ya kiliturujia hayawezi tena kubatilishwa.Kazi iliyopo ni kukuza na kulinda liturujia ambayo imekabidhiwa na sheria ya Kitume ya Vatican na Maaskofu wa majimbo ambao wana wajibu; Aidha Baba Mtakatifu anaongeza, anaamini madaraka hayo katika kipindi hiki, pamoja na hayo wanahusishwa  hata mipango ya kitaifa, kijimbo katika miundo ya liturujia ya wachungaji, taasisi za mafunzo na seminari. Katika sekta hii ya mafunzo imesimikwa nchini ya uangalizi Italia katika Kituo cha Kiliturujia na juhudi zake ikiwa ni pamoja na Wiki ya Kiliturujia ya mwaka.
Baada ya kupitia kukumbuka safari ya historia ya Liturujia amependa kugusia mambo kadhaa juu ya kauli mbiu ya Wiki ya Liturujia isemayo Liturjia hai katika kanisa hai”. Liturjia ni hai kwasababu ya uwepo wa Yule aliyekufa na akaharibu kifo chetu, aidha kufufuka kwake akarejesha maisha yetu. Bila uwepo halisi wa fumbo la Kristo, hakuna uhai waliturujia. Ni kama vile bila mapigo ya moyo hakuna maisha ya binadamu na  hivyo bila moyo unaopiga hakuna maisha.
Kinachofafanua Liturujia ki ukweli ni utekelezaji katika ishara za watakatifu, ukuhani wa Yesu Kristo, katika kutoa maisha yake hadi kunyosha mikono yake juu ya msalaba. Ukuhani huo unajieleza hadi sasa kwa njia ya ibada na sala na zaidi katika mwili na damu yake, lakini pia katika  ukuhani mwenyewe wakati wa kutangaza Neno la Mungu na katika muungano wa sala kwa jina lake
Kati ya ishara zinazoonekana katika fumbo  ni altare . Hiyo ni  ishara ya Kristo jiwe hai lililokataliwa na watu lakini limekuwa msingi wa kiroho  unaaotolewa na Mungu aliye hai katika Roho ya kweli. Kwa njia hiyo altare ni kituo ambacho makanisa yote hukutana na kutoa mawazo na maombi yao. Altare  imepakwa mafuta ya Krisma, inafukiziwa ubani, inabusiwa na kuheshimiwa,na  kwa upande wa madhabahu kwa kugeukia upande wa waumini, mapadre na waamini wote wanao unganika katika meza hiyo. Juu ya altare inatolewa dhabihu ya Kanisa ambayo ni dhabihu ya sadaka ya Kristo. Katika altare ndipo mkate  wa maisha unamegekea na kikombe cha wokovu.
Liturujia ni maisha ya watu wote wa Kanisa. Kwa asili Liturujia ni watu wote na siyo kuhani tu kama mafundisho yasemavyo. Ni tendo kwa ajili ya watu pia  watu wenyewe. Kama inavyokumbusha mara nyingi sala za  kiliturujia ni tendo ambalo Mungu mwenyewe anajidhihirisha kwa watu wake, ni tendo la watu hao kusikiliza Mungu anakiongea. Watu wanafanya hivyo kwa kusifu, kuomba na kupokea chem chemi ya maisha na huruma ambayo inatoa watakatifu na ishara.Kanisa ndani ya  sala inawapokea wote wenye  moyo wa kusikiliza Injili bila kuwa na ubaguzi: wanaalikwa wote wadogo kwa  wakubwa, matajiri na maskini, watoto na wazee, wagonjwa na wenye afya , wenye haki na wadhambi. Ni kama mfano wa umati wa watu wengi  wanao adhimisha liturujia katika madhabau ya mbingu(Uf 7,9). Ni makutano katika Kristo bila kujali umri rangi, kabila au utaifa. Msisahau kabisa kuwa Liturujia inajieleza kwa matendo ya huruma kwa watu wote wa Mungu kwa njia hiyo ni lazima kukua na kuhamasisha  upendo na ukarimu na kutia moyo kwa njia ya liturujia.
Liturujia ni maisha na siyo wazo tu la kutambua. Matoke yake ni kufanya uzoefu wa namna ya kufikiria na mtindo wa kuishi, siyo tendo la kujibinafsisha au kuwa na  sanduku la mawazo juu ya Mungu. Madhimisho ya Liturujia hawali ya yote ni mafunzo  ya kutambua au maadhimiho kutimiaza asili yake kwa maana ya kutokuwa na   utofauti, ni chem chemi ya maisha na mwanga wa safari ya imaniTafakari ya kiroho ni kitu tofauti na Liturujia, ambayo ni fumbo la mungu. Ni kuacha ujikite ndani zaidi  katika mafumbo ya Mungu. Kuna utofauti mzuri kati ya kusema Mungu yupo na kusikia kuwa Mungu anakupenda jinsi ulivyo. Katika sala ya Liturujia upo uzoefu  wa muungano wenye maana na siyo tu mawazo ya kijuu juu, bali ni tendo ambalo sisi ni wakala wa Mungu,au  Kristo na Kanisa. Maadhimisho na sala, kwa namna ya kueleza vizuri ni shule ya maisha ya kikristo, iliyo wazi kwa wote wenye kuwa na masikio, macho na mioyo iliyofunguka kupokea wito na kuwa  mitume wa Yesu.
Kanisa hakika ni hai hakina ni hai, na uhai wake katika Kristo, inajitolea maisha yake, ni mama, ni utume, Kanisa linatoka kwenda kukutana na jirani, linakuza na kuhamasisha, linatoa huduma bila kufuata tamaa za ulimwengu huu ambao unafanya dunia kuwa tasa. Kwa njia hiyo  kuadhimishwa fumbo takatifu, katika kukumbuka Maria anayeimba wimbo wa kusifu ni kutafakari yeye kama usafi unaotaminiwa kuwa jinsi ulivyo.
Hatimaye, hatuwezi kusahau kuwa utajiri wa Kanisa katika sala kama "Katoliki" ni zaidi ya la Roma, ibada ya misa ambayo licha ya kuwa kubwa, siyo peke yake. Utulivu wa tamaduni  wa  ibada za Mashariki na Magharibi, kwa pumzi ile ile ya Roho inatoa sauti katika Kanisa moja kuomba kwa njia ya Kristo pamoja na Kristo na ndani Kristo,heshima  na  utukufu wa Mungu Baba na wokovu dunia nzima.
Amemalizia Baba Takatifu akiwashukuru uwepo wao na kuwatia moyo wahusika wa Kituo cha Utendaji cha Kiliturujia wandelee kushiriki imani na mwelekeo halisi wa tangu mwanzo,katika huduma ya sala kwa watu watakatifu wa Mungu. Uzoefu wa muda mrefu wa Wiki yaLiturujia ambayo imefanyika katika majimbo mengi ya Italia pamoja na gazeti la Liturujia, imesaidia kutokudhoofika kwa Liturujia balia kuhamasisha liturujia kwa upya katika maisha ya parokia, seminari na jumuiya za kitawa.Magumu haya kukosekana, lakini hata furaha pia! Kwa njia hiyo anawaomba tena wazidi kuwasaidia makuhani wote wa daraja na , waimbaji, wasanii, wanamuziki kushirikiana ili Liturujia iweze kuwa chemchemi  ya maisha hai ya Kanisa.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican


Chapisha Maoni

 
Top