0
Baba Mtakatifu Francisko alitangaza tarehe 1 Septemba ya kila mwaka kuwa ni Siku ya Kuombea Viumbe Hai Duniani, kwa upande wa Kanisa la Kiorthodox, tarehe hii ilitangazwa tangu 1989, kwa njia hiyo hata makanisa mengine pamoja na  Baba Mtakatifu Francisko wameungana kwa pamoja hivi karibuni mwaka 2015. Kipindi cha kuombea huduma ya Viumbe kimewekwa muda wa mwezi mmoja ambapo kinamalizika tarehe 4 Oktoba ikiwa ni sikukuu ya Mtakatifu Francisko wa Assisi.  

Tarehe 6 Agosti 2015 ilichapishwa Barua ya Baba Mtakatifu Francisko ambayo ni mwongozo wa huduma ya viumbe. Katika barua  hiyo Baba Mtakatifu Francisko amehimiza Kanisa Katoliki kuungana na Mkuu wa Kanisa la Kiekumeni la Kiotodosi, Patriaki Bartholomeo wa kwanza, ambaye kwa namna amekuwa na moyo wa kujali hudma ya viumbe hai. Kwa njia hiyo Wakatoliki wote  na waanglikani wote wanaunganika kwa pamoja kuadhimisha siku hiyo. Katika kipindi hicho cha mwezi mzima, dunia nzima inafanya matendo ya dhati katika huduma kwa viumbe. Dunia inawakilisha milioni 500 za wakristo ikiwa ni pamoja na umoja wa waanglikana na jumuiya nyingine za Kanisa. 
Hata Baraza la Maaskofu nchini Italia wanasisitiza katika kipindi  cha huduma ya viumbe kuanzisha matukio mbalimbali ya kuenzi mwezi huo, ambapo wanatazamia kuadhimisha kwa pamoja  wakatoliki na waanglikana kwa namana ya pekee pia wakiwa wanaadhimisha mwaka wa 500 wa mageuzi. Halikadhalika kutakuwa na matukio mbalimbali dunia nzima ambayo tayari wameonesha ratiba hizo kama vile nchini Ufilippini mahali ambapo Kardinali Antonio Tagle ataadhimisha misa ya huduma ya Viumbe, nchi ya Uswis, ni mahali ambapo waanglikani watafanya huduma ya pamoja kusafisha maji machafu,na  Marekani ni mahali ambapo watawa wote wanaalikwa kufanya maombi katika maeneo yenye mionzi.
 Anayetaka kujua zaidi anaweza kuona hapa: http://it.seasonofcreation.org.
Aidha taarifa inasema kuna ishara nyingine ambazo zitafanyika kwa mfano huko Assizi, tarehe 1 Septemba katika Madhabahu moja Askofu Domenico Sorrentino, Askofu wa Assizi-Nocera-Guardo Tadino, pamoja na Askofu wa Gubio Mario Ceccobelli, wakiwa waamini wa jumuia nzima mahalia, watakumbuka ishara ya Kijana Francisko aliye vua nguo zake ili kuweza kujikabidhi kwa Mungu kabisa na ndugu zake, kutoa Farasi yake ya kivita na kuanza hija ya kutembea na miguu kutoka Assizi hadi Gubio.Ishara hizo ni pamoja na za jumuiya nyingi duniani zitakazofanyika kipindi chote cha mwezi mzima katika kaadhimisha  Siku ya Dunia ya Sala ya Kuombea Huduma kwa viumbe.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
Chanzo cha habari ni http://sw.radiovaticana.va

Chapisha Maoni

 
Top