Tarehe 26 Agosti Kanisa Katoliki linafanya kumbukumbu ya Liturujia ya Mama Maria wa Czestochowa nchini Poland. Mwaka huu ni maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na jubilei ya miaka 300 tangu kuwekwa taji juu ya kichwa cha picha ya miujiza ya Maria iliyotokea tarehe 8 Septemba 1717 ambayo iko katika Madhabahu ya Jasna Gora. Katika tukio la maadhimisho hayo, naye Baba Mtakatifu Francisko, ameshiriki nao kiroho pia kwa kuwatumia ujumbe kwa njia ya Video. Baba Mtakatifu anaonesha furaha kubwa hasa kwa wote waliofanya hija ya safari ndefu kuweza kuifikia siku hiyo pamoja na maaskofu ,
mapade na mji wote wa Kiroho wa nchi hiyo.
Kama Czestochowa katikati ya moyo wa Poland, ina maana ya kwamba Poland ina moyo wa umama, maana yake kila pigo la maisha ni pamoja na mapigo ya Mama wa Mungu. Wote wamekabidhiwa kwake yeye wakati uliopita, uliopo na a endelevu fuhaha na uchungu wa maisha yao binafsi na kwa nchi yao pendelevu: Baba Mtakatifu anaongeza, hilo ni jambo jema. Aidhaanasema jinsi ilivyo vema kwake kukumbuka sikukuu hiyo aliyoweza kuifanya pamoja nao wakati wa ziara yake ya kitume nchini Poland, akiwa chini ya mtazamo wa Mama, hasa alipojikuta anainua uso wake kutazama uso wa Maria na kumkabidhi katika moyo wake yote yaliyokuwa katika mioyo yao wote. Kwa njia hiyo anasema, bado anayo kumbukubu ya wakati ule na furaha ambayo naye aliweza kushiriki alipokwenda kama muhujaji na kuadhimisha misa chini ya mtazamo wa mama Maria ikiwa pia ni katika kuadhimisha miaka 1050 ya kuzaliwa kwa nchi ya Poland.
Katika fursa ya neema inawakusanya watu wengi kwa siku hii ambapo kwa miaka 300 iliyopita,Papa wa wakati ule alikubali kuweka taji la kipapa katika picha ya Mama wa Jasna Gora ambaye ni Malkia wenu. Ni heshima kubwa kuwa na Mama Malkia, Mama wa Malaika na watakatifu wanao tawala na utukufu mbinguni. Pamoja na hayo bado ni furaha zaidi kutambua kuwa mnaye Malkia , mama wa kupenda kama Mama ambaye mnamwita Mwanamke. Picha Takatifu inaonesha kwa dhati Maria siyo Malkia aliye mbali anayekaa katika kiti cha kimalkia, yeye ni Mama anayekumbatia mtoto wake, kwa namna hiyo hata sisi wote tu watoto wake. Ni mama aliye karibu hapotei katika mitazamo yetu, mama mpendelevu anaye tushika mkono katika safari yetu ya kila siku.
Ni matashi mema ya kuweza kuwa na uzoefu huo katika maadhimisho ya jubilei ambayo mnafanya: Baba Mtakatifu anaendelea, iwe ni kipindi cha kujihisikuwa kuwa hakuna yoyote aliye yatima kwa njia hiyo kila mmoja anaye Mama, Malkia asiyeshindwa wema wake.Yeye anatutambua na kutusindikiza katika mtindo wake wa dhati wa kimama, wa unyenyekevu na wakati huo huo akiwa jasiri:halikadhalika haingilii kamwe bali, daima ni imara siku zote kwa wema, mvumilivu mbele ya mabaya na ni mwaharakati wa kukuza mapatano.
Anamalizia ujumbe kwa njia ya video akisema, Maria awape neema ya kupata furaha pamoja kama familia walioungana kumzunguka Mama huyo. Na katika moyo huo wa umoja wa Kanisa, unakuwa na nguvu ile ya mshikamano wa kuunganisha nchi ya Poland na Kharifa wa mtume Petro. Amewabariki na kuwaomba sala kwa ajili yake.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni