0

"Inatosha kupiga ngoma katika vita", ni kichwa cha waraka  uliotiwa na sahini na Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama ambaye ni askofu Mkuu wa Jimbo la Jose na  Askofu Wiliam Amove Avenya, Askofu wa Jimbo la Gboko, wote kwa pamoja wkiwa ni Rais na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Nigeria kwa niaba ya maaskofu wote nchini humo katika kuelezea wasiwasi wao mkubwa  wa serikali ya shirikisho la Nigeria  kwasababu ya mivutano na ghasia za makabila yanayoendelea kujitenga na jamii kwa miaka 50 tangu kuzuka kwa vita vya Biafra 1967-1970.


Katika  migogoro hiyo Maaskofu wananukuliwa na Shirika la habari la Fides kwamba wanatoa onyo, ni lazima kujifunza kutokana na uzoefu wa kutisha wa vita vya kiraia, pamoja na uharibifu wa idadi kubwa ya maisha na mali ambazo madhara bado ni wazi kwa siku hizi,aidha ili kuepukana mvutano wa sasa unaoweza kusababisha janga jipya la kitaifa. Maskofu wanaandika; bila shaka kwa miaka miwili ya karibuni maisha ya taifa la Nigeria limeona kuongezeka machafuko  na mivutano ya kikabila na kikanda ambayo yameongeza sera za hawali za kisiasa,na mivutano ya kidini kikabila na kijamii. Mivutano hiyo naonesha picha dhahiri ya taifa kutikiswa ambapo idadi  ya watu mbalimbali wanahisi kutengwa au kubaguliwa.
Miongoni mwa wale walio tengwa kwa namna ya pekee  sehemu kubwa  hasa ni kizazi cha wakazi vijana , hiyo siyo siri kwa mtu yoyote  kuwa hali ya Nigeria haitii moyo kwa kizazi cha vijana endelevu. Hiyo imesababishwa na uchoyo na ufisadi  katika madaraja ya kisasa walio wazee aabao wanazidisha hasira kwa vijana. Hali kadahali Maaskofu wathibitisha kuwa demokrasia ya kweli inawezakana iwapo wataimarisha tabaka la kisiasa, wasomi na wazee kuifikia makubalino ya kuhakikisha mshikamano wa kitaifa na hali ya uchumi wa umoja kwa wote.

Waraka wa Maaskofu wa Nigeria unatoa onyo kuwa;kwa wale wanao hisi kubaguliwa na kutengwa,na kuonewa hata hivyo ni lazima wasichukue fursa ya haki na  uhuru wao wa kujieleza kwa njia ya kutumia uchochezi wa kutishia umoja wa maisha ya nchi. Kwa njia hiyo Maaskofu wanatoa wito wa mwisho kuwa "inatosha kupiga ngoma ya vita".Vita ni ugonjwa wa upepo ambao hauleti faida fulani kwa mtu yoyote.Ni lazima kushiriki zaidi katika kujenga mawasiliano na mazungumzo ndani ya mfumo wa demokrasia ambayo inakataa chuki, kutokuvumilana au kujiona mwenye hali  bora zaidi ya wengine.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

Chapisha Maoni

 
Top