Anawakaribisha ndugu wote wanachama kutoka dunia nzima wa makundi ya wasanii wa maonyesho ya mitaani, wawakilishi wote wa Chama cha kitaifa cha maonyesho na anashukuru pia Rais wa chama kwa hotuba yake. Aidha kuwapa salam zake familia zao na marafiki ambao hawakupata fursa hiyo ya kuwapo, kwa namna ya pekee watoto wazee na wagonjwa.
Ni utangulizi wa maneno yake Baba Mtakatifu Francisko wakati alipokutana na wasanni wa mitaani kutoka ulimwenguni kote Ijumaa 15 Septemba 2017.Baba Mtakatifu Baba Mtakatifu anatambua
ugumu wa maisha yao kwani daima ni watu wanaozunguka sehemu mbali mbali za dunia kwa kazi ngumu na kumbe anasema siyo rahisi kuwa na makazi ya kudumu. Anatambua pia matatizo makubwa wanayokabiliana familia zao .Hiyo ni pamoja na kuhamisha vyombo na zana katika viwanja ili wapate nafasi kwa mujibu wa shughuli zao; wakati huo wanalazimika kukaa nje ya mji , wakati mwingine kuna jumuiya daima ambazo hazithamini jamii ya usanii wao wa maonesho.
Baba Mtakatifu anawatia moyo wasikate tamaa bali wandelee mbele na katika safari hiyo ya changomoto na kuhakikisha kwamba wanajitahidi kuboresha imani yao yao kwa kupokea Sakramenti za Kanisa; kwa kurithisha upendo wa Mungu kwa watoto na jirani zao pamoja na kutambua kwamba, Kanisa linawajali na kuwathamini na linataka kusaidia kuondokana na maamuzi mbele yanayowasukumizwa pembezoni mwa jamii zao. Anawataka kutekeleza dhamana na wajibu wao kwa furaha, kwa umakini mkubwa, daima wakiwa na imani kwa Mwenyezi Mungu anayewasindikiza daimakatika maisha yao.
Njia yenu ambayo Mungu anaangaza kwa imani , yaani imani yao wanayoishi zaidi katika familia na ndiyo hawali ya yote muhimu kwa maana anasema, familia inayotembea na Mungu, kwa kuongoza na imani na zawadi. Ni imani ambayo pia inapatikana katika maparokia kwa kupitia sehemu ambazo ni kiini cha kiroho.
Baba Mtakatifu Francisko anawakumbusha alipokutana na ulimwengu wa kisanii wa mitaani mwaka jana, aliwaeleza kuwa, wao ni wafanyakazi wa mashuhuri wa sikukuu na mshangao wa uzuri, na aliwaalika kukuza na kuongeza hisia za matumaini na uaminifu. Ni kweli, kwamba Wasanii hawa ni chemchemi ya faraja, amani, upendo, mshikamano, urafiki na matumaini kwa watu waliokata tamaa. Hata hivyo anasema, anaungama kwamba naapendelea usanii wao unaotoa arufu nzuri ya mshangao ambao lakini ni tunda la uwajibikaji na masaa mengi ya kazi ngumu. Hakika michezo yao haina mwisho wa kuleta mshangao, inaleta furaha tamu kwa wadogo na wakubwa.
Ni wito ambao mara moja unakuwa utume, kwasababu ni utume wa kijitoa kwa watu , watoto , lakini pia kwa watu wazima na wazee, ni fursa ya kujifurahisha hata kiafya, na safi. Na ndani ya wito huu na utume, inawezekanaje pasiwepo mkono wa Mungu? Ni swali : Baba Mtakatifu anauliza, na kujibu kuwa, Mungu anatupenda na anataka tufurahi.
Mahali palipo na furaha nyepesi , safi , kuna ishara zake. Kwa njia hiyo iwapo watatambua kutunza maadali haya , uaminifu huu na unyenyekevu, wao watakuwa wajumbe wa furaha ambayo Mungu hupendezwa nayo, na ambayo inatoka kwake. Baba Mtakatifu anamalizia hotuba yake kwa kuwakabidhi chini ya ulinzi wake mama Maria , awasindikize daima katika safari yao ya kuhama hama katika usanii wao . Anawabariki kwa moyo wote hata wapendwa wao na kazi zao, wakati huo huo wasisahau kusali kwa ajili yake.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa yak swahili ya radio Vatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni