0
Mwili wa Sr Bernadeta ulifunguliwa mnamo tarehe 24 January, 2012 mbele ya maaskofu wa metropolitani ya Songea ambayo inahusisha majimbo  nane ambayo ni Songea, Njombe, Mbinga, Mbeya, Iringa,Tunduru Masasi,Lindi na Mtwara.

Siku ya ufukuzi wa Kaburi hilo watu wengi walivutika kuja kuona kilichomo kani moja, mni jambo geni lakini pili wengi walipatwa na shahuku ya kujua nini kinaweza kitakachoweza kupaatikana kwa mtu aliyekufa miaka hamsini(50) iliyopita.
 
 
“Mwanzoni tulidhani hakutakuwa na kitu baada ya kukuta mchwa wengi lakini tulipochimba zaidi tlishangaa kuiona mifupa yake, punje za rozari na msalaba” Alisema Fr Francis Shawa ambaye yuko kwenye kamati ya mchakato huu.

Kwa sasa masalia hayo yamehifadhiwa katika kikanisa cha Askofu Mkuu mwashamu Norbert Mtega wa jimbo kuu katoliki la Songea. Kwa sasa utaratibu unaofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Songea wa kujenga mahali rasmi ili kuweka masalia ndani ya Kanisa.
 
 Hivi karibuni rafiki Vicenza-Marie alipata nafasi ya kuongea na Baba Askofu Norbert Mtega Kurasini Dar eslaam na katika maongezi hayo baba pia aliongelea swala la uhifadhi wa masalia. “Itapasa pia masalia ya Mtumishi wa Mungu yaliyoko Chipole yajengewe mahali maalum pa kuyaweka ndani ya Kanisa, kwani ni muhimu na ni lazima kisheria kufanya hivyo ili kutoa fursa kwa waamini na watu wengine kusali mbele ya Masalia ya Mtumishi wa Mungu na kufanya hija yao huko”
 
 
Vilevile baba alisema ya kwamba  “Pamoja na sehemu hizo mbili yalipohifadhiwa masalia hayo, itabidi tutengeneze upya kaburi lake pale Peramiho, ili hapo pia pawe ni mahali maalum pa hija kwa watu binafsi wanaotaka kuhiji. Hivyo, hija zitaweza kufanyika: Songea, Chipole, Peramiho na Luwawazi-Likuyufusi, mahali alipozaliwa,” 
Shime shime marafiki pelekeni shida zenu;magonjwa, masomo,matatizo ya uzazi na kadhalika kwa Mungu kupitia maombezi ya sista huyu ili aweze kuingia katika orodha ya watakatifu. Pia tunaomba kuchangia mchakato huu kwa akaunti ya jimbo la Songea ili kufanikisha mchakato huu ambao nighali sana.

Katika upendo wa Kristu,

Chanzo cha habari http://bernadetambawala.blogspot.com/2012/04/masalia-ya-mwili-wa-sr-bernadeta.html
Vicenza-Marie

Chapisha Maoni

 
Top