Baba Mtakatifu amemteua Askofu mpya wa Jimbo la Franceville nchini Gabon, Padre Jean-Patick Iba-Ba, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Gombera wa Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mtakatifu Augustin” huko Libreville Gabon. Padre Jean-Patick Iba-Ba, alizaliwa tarehe 18 Aprili 1966 huko Libreville, na kuanza shule ya msingi mnamo mwaka 1973 - 1979 huko Port-Gentil Gabon.
Aliendelea na masomo ya Sekondari kuanzia 1979 -1989, huko Libreville. Majiundo ya upadre, alitumwa na Askofu Mkuu wake huko Seminari kuu ya Kardinali Emile Biayenda huko Brazzaville, mji Mkuu wa Congo. Mwaka 1993-1998 aliendeleza na masomo ya Taalimungu katika
Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniano Roma.
Alipata daraja Takatifu la upadre tarehe 19 Julai 1999 katika Jimbo Kuu la Libreville. Na baada ya upadrisho alifanya utume mbambali kama ifuatavyo: kama msaidizi wa Gombera katika Seminari kuu ya Mtakatifu Augustin huko Libreville kuanzia 1998-1999 ; Gombera wa Siminari ndogo ya Mtakatifu Jean wa Libreville mwaka 1999-2001 na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Michel wa Ndjole mwaka 2001-2004.
Mwaka 2004-2009 alirudi Roma kuendelea na masomo na kupata digrii ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniano. Mwaka 2009-2012 kuwa makamu wa Gombera ya Seminari Kuu ya Augustin wa Libreville; mwaka 2010-2012 Mkurugenzi wa Shule Katoliki nchini Gabon na Msimamizi Mkuu wa Taasisi za Elimu Katoliki. Na tangu 2012 hadi uteuzi wake amekuwa Gombera wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustin nchini Gabon.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni