Hapo jana (Ijumaa tarehe 3 Novemba), Baba Mtakatifu Fransisko
ameadhimisha misa Takatifu kwa ajili ya kuwaombea marehemu wote
makardinali na Maaskofu waliokufa kwa kipindi cha mwaka huu. Katika
mahubiri yake anasema, kwa mara nyingine tena Liturujia ya siku
inatuweka katika hali halisi ya kifo na kukumbusha watu tulioshi nao
karibu pia wale walio tutendea mema. Lakini vile vile Liturujia
inaongeza matumaini yetu kwa ajili yao na hata sisi wenyewe.
Somo la kwanza linaeleza juu ya matumaini ya kufufuka kwa wale wenye
haki.Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine
wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. (Dn 12,2).
Baba Mtakatifu anaongeza, kifo ndiyo upeo wa mwisho kuondokana na
makona kona ambayo yako mbele yetu katika ulimwengu huu: Njia ya maisha
inayotupeleka katika mungano na Mungu au njia ya kifo inayotupeleka
mbali na Yeye. Wangi ambao watafufuka katika maisha ya milele, wako
wanasubiri kama wale ambao Kristo amemwaga damu yake kwa ajili yao. Hawa
ni undi kubwa kwa neema ya huruma ya Mungu ambayo inajieleza katika
hali halisi ya maisha ambayo yana ushindi juu ya kifo kwakuwa kuna
ufufuko.
Injili inaimarisha matumaini yetu: “ Mimi ni mkate wa uzima ushukao
mbinguni, kila aulaye mkate huo ataishi milele (Yh 6,51). Hayo ni maneno
yanayoeleza sadaka ya Kristo Msalabani. Yeye alikubali kifo kwa ajili
ya kuwakomboa watu ambao Baba yake alimkabidhi, ni watu ambao walikuwa
wamekufa katika utumwa wa dhambi. Yesu amekuwa kaka yetu na kushiriki
maisha yetu hadi kifo. Ni kwa njia ya upendo wake , alivunja minyororo
ya kifo na kutufungulia mlango wa maisha. Kwa kulishwa mwili wake na
damu yake sisi sote tunaungana na upendo wake mwaminifu, ambao
unatupatia matumaini ya ushindi hadi mwisho dhidi ya ubaya, mateso na
kifo.
Kwa nguvu za agano la Mungu kwa upendo wa Kristo sisi sote tunatambua
kuwa umoja kwa walio kufa syo wa kufikirika, bali ni utashi, ni jambo
halisi. Imani tunayokiri katika ufufuko inatupelekea kuwa watu wa
matumaini, Baba Matakatifu anasisitiza, na wala siyo kuhangaika, sisi ni
watu wa maisha na siyo wa kifo , kwasababu Yeye anatufariji na kutoa
ahadi za maisha ya milele yanayotokana na umoja na Kristo Mfufuka.
Imani hii inayowaka ndani mwetu kwa njia ya Neno la Mungu inatusiadia kuwa na tabia ya matumaini mbele ya kifo. Hiyo ni kutokana na kwamba Yesu mwenyewe alituonesha kuwa kifo hakina neno la mwisho bali ni upendo wa huruma ya Baba yake ambaye anajionesha kwetu na kutufanya tuishi katika muungano naye daima.
Imani hii inayowaka ndani mwetu kwa njia ya Neno la Mungu inatusiadia kuwa na tabia ya matumaini mbele ya kifo. Hiyo ni kutokana na kwamba Yesu mwenyewe alituonesha kuwa kifo hakina neno la mwisho bali ni upendo wa huruma ya Baba yake ambaye anajionesha kwetu na kutufanya tuishi katika muungano naye daima.
Tabia msingi ya maisha ya kikristo ni matarajio ya mwisho ya kukutana na
Mungu, kama zaburi ( 42,3) isemavyo : Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu,
Mungu aliye hai, lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Baba
Mtakatifu anaongeza kusema, hayo ni maneno yanaojieleza kwa namna ya
kutoa mshangao wa matarajio, kwa maana ya kuona kiu ya upendo, ya uzuri
na hata ya furaha na matumaini kwa Mungu.
Maneno ya mzaburi yaliyojiweka kama muhuri katika mioyo ya makardinali
na maaskofu ambao leo hii wanakumbukwa: wao wameondoka baada ya
kuhudumia Kanisa na watu wa Mungu walio kabidhiwa , na katika mtazamo wa
umilele. Baba Mtakatifu anasema, tukiwa tunashukuru Mungu kwa huduma
yao na ukaribu walioonesha katika Injili na Kanisa, ni vema kurudia na
mtume Paulo kuwa matumaini hayakatishi tamaa, na kwa maombezi ya Maria
maa Yetu Mtakatifu atusaidie ili tuweze kushiriki katika meza ya Bwana ,
ambayo kwa imani na upendo tumeonja kipindi chote cha hija ya hapa
duniani.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni